Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wakiwa na uwezo wa kufanya maamuzi ni ushindi kwa kila mtu:Guterres 

Wanawake wabunge Afghanistan wakiingia Bungeni (Wolesi Jirga )
UN Photo/Eric Kanalstein
Wanawake wabunge Afghanistan wakiingia Bungeni (Wolesi Jirga )

Wanawake wakiwa na uwezo wa kufanya maamuzi ni ushindi kwa kila mtu:Guterres 

Wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amefanya mkutano wa kimataifa na mamia ya wawakilishi kutoka asasi za kiraia kumulika suala la wanawqake baada ya mkutano wa kila mwaka kuhusu hali ya wanawake duniani ambao hufanyika mwezi Machi kufutwa mwaka huu kwa sababu ya janga la corona au COVID-19. 

Mkutano huo unaofanyia kwa njia ya mtandao unajikita na mada ya wanawake na COVID-19. Mkutano huo umehudhuriwa pia na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka ambaye amezungumzia suala la kuwajumuisha wanawake na wasicha na watu kutoka kila kona ya dunia na suala zima la uongozi. 

Hofu zilizopo 

Katika taarifa yake kwa mkutano huo Bi. Ngcuka amesisitiza kwamba, “ni wakati wa kutambua sauti za wale wasiojumuishwa na wale ambao mahitaji yao ndio malengo ya hatua za wanaharakati katika nyanja zote.”  

Ameongeza kuwa asasi za kiraia na harakati za wanawake ni washirika wakubwa katika juhudi za kubaini na kukabiliana na pengo la usawa ambalo limeongezeka sana wakati wa janga la COVID-19. 

COVID-19 imeongeza changamoto kwa wanawake 

Naye Katibu Mkuu Antonio Guterres amesisitiza kwamba, “janga la COVID-19 limeanika na kuongeza vikwazo vinavyowakabili wanawake katika kufikia haki zao na uwezo wao.” 

Ameeleza kwamba hatua kubwa zilizopigwa zimerudi nyuma na itachukua miaka na hata vizazi kurejea natika mafanikio hayo lakini kwa kuchukua hatua maalum inawezekana . 

Kwa mantiki hiyo Bwana. Guterres amesema “Wakati wanawake wana uwezo wa kufanya maamuzi, ni ushindi kwa kila mtu” akisistiza ujumuishwa wa kundi hilo katika ngazi ya maamuzi. 

Kulinda haki za wanawake 

Katika taarifa yake pia Katibu Mkuu amesema kwamba kulinda haki za wanawake na wasichana wakati huu wa janga la corona ni kipaumbele cha hali ya juu cha Umoja wa Mataifa. 

Amefafanua kwamba katika awamu ya kwanza, kipaumbele ni kuchukua hatua za afya, katika hatua ya pili ya kukabiliana na janga hilo , lengo ni kupunguza athari za kuchumi na kijamii zilizosababishwa na mgogoro huu wa kimataifa n ani kuanzia kwa uwekezaji kwa wanawake wanaofanyakazi katika sekta rasmi na zisizo rasmi. 

Guterres amesisitiza kwamba katika awamu ya tatu ya hatua, kipaumbele ni kujikwamua vyema kutoka kwenye janga hili na kujenga mustakabali bora. 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema janga hili linaonyesha kwamba karne ya mfumo dume imesambabisha wanaume kuitawala dunia kwa utamaduni ambao unawaumiza wanawake, wanaume, wasichana na wavulana. 

Ombi maalum 

Katibu Mkuu ameomba kwamba katika dharura ya mgogoro huu wanawake wanapaswa kuwa na fursa sawa kwa uongozi na uwakilishi. 

Kwani amesema hivi sasa ni salimia 8 tu ya viongozi wakuu wan chi na serikali ndio wanawake. 

Wanawake wabunge ni chini ya asilimia 25 ya wabunge wote duniani na ingawa asilimia 70 hadi 90 ya wahudumu wote wa afya ni wanawake , chini ya theluthi moja ya wahudumu hao ndio wanaoshiriki katika ngazi ya maamuzi yanayoathiri  katika sekta hiyo.