Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa kidijitali utawawezesha raia kudhibithi fedha kwa ajili ya SDG’s:UN

Wataalam wa Turkmenistan wanachambua twakimu ya uchambuzi.
© World Bank
Wataalam wa Turkmenistan wanachambua twakimu ya uchambuzi.

Uchumi wa kidijitali utawawezesha raia kudhibithi fedha kwa ajili ya SDG’s:UN

Ukuaji wa Kiuchumi

Kikosi kazi cha Umoja wa Mataifa kilichoundwa kutathimini hatari na faida za uchumi wa kidijitali kimehitimisha kwamba uchumi huo unaweza kuwa na atharinzuri za mabadiliko makubwa katika maendeleo endelevu na kuwawezesha raia ambao ni walipa kodi na wawekezaji.

Hayo yamo katika ripoti iliyopewa jina “Fedha za raia:kukumbatia masuala ya kidijitali kwa ajili ya kufadhili mustakbali endelevu” ambayo imetolewa leo na kikosi kazi hicho kilichoundwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. 

Kikosi kazi hicho ambacho kinaongozwa na Achim Steiner mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na kujumuisha watu wengine muhimu kutoka sekta za teknolojia, taasisi za fedha, serikalini na vyombo vya Umoja wa Mataifa kilianzishwa rasmi mwaka 2018 ili kuimarisha uelewa wa faida na hasara za mabadiliko ya haraka ya teknolojia ya masuala ya kifedha na sekta za kidijitali za fedha. 

Mpango huu ni sehemu ya mkakati wa mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia katika ufadhili kwa ajili ya ajenda ya 2030 ambayo ni kitovu cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mustakabali bora wa wat una sayari dunia. 

Ufadhili unaohitajika 

Katibu Mkuu Guterres aalisema mwaka 2018 kwamba fedha zinazohitajika kwa ajili ya mchakato huo ni kati ya dola trilioni 5 hadi 7 kwa mwaka. Ripoti ya kikosi kazi hicho kuhusu fedha za watu wa kawaida kabisa imesema kuingia katika masuala ya kijdijitali kutatoa njia ya kukidhi gharama hii inayotabiriwa. 

Wakati wa kuwasilisha ripoti hiyo Katibu Mkuu Guterres ameongeza kuwa “Teknolojia ya kidijitali ambazo zinafanya mapinduzi katika masoko ya fedha inaweza kuwa chachu kubwa katika kutimiza malengo ya pamoja. Kikosi kazi cha masuala ya kidijitali ya fedha kwa ajili ya maendeleo endelevu SDGs, ni msukumo katika kukumbatia mapinduzi ya kidijitali.” 

Athari zinazoendelea za COVID-19 

Wakati wa janga la COVID-19 umaarufu wa nyenzo za kidijitali uliongezeka na kuonyesha uwezekano wa masuala ya kidijitali ya fedha kutoa ahuweni kwa mamilioni ya watu kote duniani, kusaidia biashara na kulinda ajira na maisha ya watu. 

Naye mkuu wa UNDP bwana. Steiner akijibu swali kuhusu suala hilo amesisitiza athari za janga la COVID-19 na kusema “Mambo ambayo tuliyapanga kufanyika katika miaka michache ijayo yalitokea ndani ya wiki chache. Janga hili limezifanya serikali kutambua umuhimu wa kukabiliana na ukomo uliozoeleka na kubaini na kufikia watu walio hatarini zaidi.” 

Kwa mfano amesema kujumuisha utumaji wa fedha kidijitali suala ambalo limesaidia mamilioni ya watu nchini Pakistan, limeunganisha shule na broadband na kuziunganisha serikali na wabunge popote waliko katika njia ambazo sasa zimeonekana kuwa ni za kawaida. 

Kupanua wigo wa simu za mkononi Steiner amesema kumeweka nyenzo muhimu na yeney nguvu ya kidijitali katika mikono ya mamilioni ya wat una kuwawezesha kufanya kazi, kuchangamana na kudhibiti masuala yao ya fedha. 

Amessitiza pia umuhimu wa kubadili mfumo wa masuala ya fedha ili kudhihirisha ukweli kwamba matrilioni ya dola za uwekezaji zinazomwagika kote duniani kimsingi zinatoka katika watu wa kawaida. 

“Raia ni wamiliki wa utajiri ambao unajumuisha malipo ya uzeeni na akiba. Kikosi kazi hiki kinataka kusisitiza ukweli kwamba raia ndio kitovu cha uchumi. Raia wanahitaji uwazi na lazima wawe na kauali za wapi michango yao ya akiba za uzeeni inakwenda. Na mbali ya faida kwa wawekezaji, pia tunataka kuona sera za faida kwa umma. Ufadhili wa kidijitali ni fursa muhimu kwa raia kujihusisha tena kwa sababu ni njia ya kukabili changamoto kama vile mabadiliko ya tabianchi.”