Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuishinde COVID-19 na tukomeshe chuki na ubaguzi:Guterres 

Viongozi wa kidini
UN Photo/Rick Bajornas)
Viongozi wa kidini

Tuishinde COVID-19 na tukomeshe chuki na ubaguzi:Guterres 

Amani na Usalama

Katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kuwaenzi waathirika wa ukatili kwa misingi ya dini na imani, ambayo kila mwaka huadhimishwa Agosti 22, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuhusu ongezeko la ubaguzi wa rangi tangu kuzuka kwa janga la corona au COVID-19 kote duniani

Bwana Guterres amesema kwamba janga la corona limekuwa likiambatana na “Unyanyapaa mkubwa na ubaguzi wa rangi unaozighubika jamii, kusambaa kwa chuki na kutupiana lawama.” 

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameorodhesha baadhi ya mifano ya kusikitisha ya ubaguzi dhidi ya dini za walio wachache kama vile mashambulizi kwa watu na maeneo ya kidini, kauli za chuki na uhalifu mwingine ukilenga watu kwa sababu tu ya dini au imani zao. 

Ili kukabiliana na ubaguzi huu Bwana. Guterres ametoa wito wa kuchukuliwa hatua zaidi kushughulikia mizizi ya kutovumiliana na ubaguzi kwa kuchagiza ujumuishwaji na kuheshimu tofaut zetu pamoja na wahusika wa uhalifu huo kuwajibishwa. 

Katibu Mkuu António Guterres  akizungumza katika msikiti wa al-Azhar  mjini Cairo akielexzea mshikamano wake na kusisitiza haja ya kupambana na janga la chuki dhidi ya wageni na mifumo yote ya chuki na ubaguzi. 2 Aprili 2019
UN Photo/Mahmoud Abd ELLatiff
Katibu Mkuu António Guterres akizungumza katika msikiti wa al-Azhar mjini Cairo akielexzea mshikamano wake na kusisitiza haja ya kupambana na janga la chuki dhidi ya wageni na mifumo yote ya chuki na ubaguzi. 2 Aprili 2019

Uhuru wa dini ni haki ya binadamu 

“Haki ya uhuru wa dini na imani imewekwa bayana katika sheria za kimataifa za haki za binadamu n ani uti wa mgongo kwa ajili ya ujumuishwaji, mafanikio na kuwa na jamii zenye amani.” Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake. 

Ameongeza kuwa serikali zinawajibu mkubwa wa kulinda haki ya uhuru wa dini na imani. 

Mkakati uliowekwa na Antonio Guterres kusaidia ni pamoja na wito wa kuchukua hatua kwa ajili ya haki za binadamu, mkakati wa kukabiliana na kauli za chuki na mpango wa hatua wa kulinda maeneo ya kidini. 

Siku hii ya kimataifa iliundwa baada ya kupitishwa azimio la Umoja wa Mataifa mwezi Mei 2019 ili kukabiliana na ongezeko la hali ya kutovumiliana na machafuko kwa misingi ya kidini au imani dhidi ya watu , viytendo ambavyo mara nyingi ni uhalifu. 

Wakati akizindua mkakati wa kupambana na kauli za chuki Juni 2019, Guterres alisema “Ongezeko la chuki dhidi ya wageni, ubaguzi wa rangi na kutovumiliana, machafuko, chuki dhidi ya Wayahudi na kupinga Uislam” vinashuhudiwa kote duniani na kwamba katika baadhi ya maeneo jamii za Wakristo zimekuwa zikishambuliwa pia. 

Mkakati huo unalenga kuuwezesha Umoja wa Mataifa kuchukua hatu za kukabiliana na “athari za kauli za chuki katika jamii” ameeleza Guterres kwa kuwaleta wat una makundi Pamoja ambao wana mitazamo tofauti , kufanya kazi Pamoja katika vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii na kuandaa muongozo wa mawasiliano.