Tunalaani vikali mauaji ya wanaharakati wa haki za binadamu Basra:UNAMI

Mwanamke aliyebeba mtoto mchanga anavuka barabara iliyojaa taka, akiwa njiani kuelekea kituo cha hudumacha afya, katika mji wa Basra wa Iraqi.
© UNICEF/UNI39964/Noorani
Mwanamke aliyebeba mtoto mchanga anavuka barabara iliyojaa taka, akiwa njiani kuelekea kituo cha hudumacha afya, katika mji wa Basra wa Iraqi.

Tunalaani vikali mauaji ya wanaharakati wa haki za binadamu Basra:UNAMI

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI umelaani vikali mauaji ya wanaharakati wawili wa haki za binadamu na mashambulizi yaw engine wawili kwenye mji wa Basra Kusini mwa nchini hiyo na kutoa wito wa kuongeza juhudi za kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria. 

UNAMI imesema Riham Yacoub Daktari waliuawa Jumatano wiki hii na kifo chake kimekuja kukiwa na maandamano mjini Basra ya kudai uwajibikaji kwa ajili ya mauaji ya mwanaharakati mwingine Tahseen Oussama ambaye aliuawa Agosti 14. 

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa Iraq na mkuu wa UNAMI Jeanine Hennis-Plasschaert leo ameonya kwamba “Mauji haya yanawasilisha tishio kubwa kwa usalama na utulivu mjini Basra ambako ni bandari kubwa ya nchi hiyo.” 

Ameongeza kuwa Watu wa Basra hawapaswi kuishi katika mazingira hayo ya hofu na vitisho. Hatua kubwa zinahitajika kutoka kwa serikali na haraka kusshughulikia hali hii. “Sheria lazima itumike kikamilifu kusaka, kuwakamata na kuwawajibisha wahusika wa mauaji hayo na kukomesha mzunguko huu wa machafuko” amesema bi Hennis-Plasschaert. 

UNAMI imesema kwamba ofisi yake ya haki za binadamu imepokea taarifa za kuaminika za mauaji ya watu hao wawili mjini Basra tarehe 17 Agosti ambapo watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walifyatulia risasi gari lililokuwa limewabeba wanaharakati wawtatu ikiwemo mwanamke mmoja, na kujeruhi wawili ambao sasa wamelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu. 

Gari linguine lililokuwa likiendeshwa na mwanamke lilifyatuliwa risasi lakini washambuliaji walilenga vibaya na halikudhurika. 

UNAMI pia imesema ingawa inatambua hatua chanya zilizochukuliwa na serikali katika kukabiliana na matukio kama hayo, inaitaka serikali kuchukua hatua zaidi kutendea haki waathirika, uwajibikaji na kuhakikisha usalama.