Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa una fursa nyingi, muhimu vijana tuwe tayari na tuwe na moyo wa kujitolea-Hilda Phoya

Hilda Phoya, mnufaika wa mafunzo kwa vitendo katika ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu
Hilda Phoya, mnufaika wa mafunzo kwa vitendo katika ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.

Umoja wa Mataifa una fursa nyingi, muhimu vijana tuwe tayari na tuwe na moyo wa kujitolea-Hilda Phoya

Malengo ya Maendeleo Endelevu

“Umoja wa Mataifa una fursa nyingi ambazo ikiwa vijana tutakuwa na moyo wa kujitolea na bidii ya kazi, tunaweza kunufaika nazo,” hayo ni maoni ya Hilda Phoya, mwanafunzi ambaye hivi karibuni amehitimisha mafunzo kwa vitendo katika Kituo cha habari za Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania. 

Katika mahojiano haya yaliyofanywa na Ahimidiwe Olotu wa Kituo hicho, Hilda anaanza kwa kueleza kilichomvutia kuchagua kwenda katika kituo hicho ili kukamilisha masomo yake ya elimu ya juu. 

"Kitu ambacho kilinivutia kuja hapa au kutuma maombi yangu hapa ni nafasi ambayo Umoja wa Mataifa wanayo siyo tu nchini lakini pia duniani kwa ujumla, niliona ni dhahiri kwangu kujifunza hasa kwa vitendo kile ambacho nimesoma darasani nimejifunza mengi , kwa kuanza nimejifunza kupiga picha za video nilikuwa sifahamu , lakini pia nimejifunza kazi mbalimbali kama  vile kituo chetu cha habari kina maktaba kwa hivyo kazi za maktaba pia nimejifunza kazi zingine za ofisi zinazohusiana na masuala ya habari na taarifa lakini pia habari nimejifunza na pia nimejifunza kwa ndani zaidi masuala ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs na pia nimepata nafasi ya kutembelea shule mbalimbali nikiwa hapa kituo hiki cha habari cha Umoja wa Mataifa. Kuweza kuzungumza na wanafunzi juu ya mambo mengi na hayo pia yamenijenga mimi kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambapo nilikuwa nafanya mafunzo yangu hapa."

Kuhusu wito wake kwa Umoja wa Mataifa katika kuendelea kuwapa nafasi vijana hususana wasichana, Hilda anasema,

"Ni jambo njema na ni jambo nzuri kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kutoa nafasi hizi kwa wanafunzi hasa wasichana ili waweze kuwasaidia ama kutusaidia mimi nikiwa mmoja wapo kuweza kutusaidia kuingia na kufanya kazi."

Na je, Hilda ana ushauri gani kwa vijana wenzake?

"Tuwe na moyo wa kujitolea tuwe na utayari na nidhamu ya kujitolea na kufanya kazi kwa bidii tuwe tayari kwa sababu kama Umoja wa Mataifa inanafasi nyingi ambazo inatoa sio tu katika kituo cha habari lakini pia katika mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kuna nafasi nyingi za vijana kujitolea kwa hivyo tuwe na utayari na nidhamu ya kujitolea. Nashukuru kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania, nashukuru Umoja wa Mataifa wote kwa ujumla na wale ambao tumefanya kazi pamoja wamekuwa msaada mzuri kwangu na wamenisaidia kwa kweli na popote ambapo nitaenda nitakumbuka mafunzo na nitaendelea kutia juhudi nitawakilisha vyema Umoja wa Mataifa kwa nafasi yangu mimi ya kuwa hapa. "