Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yateua jopo kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu Libya

Jamaa wa mfungwa analia wakati akitafuta picha yake katika hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya 1996 ambayo karibu wafungwa 1,200 walipigwa risasi na walinzi wao. (faili)
UNSMIL
Jamaa wa mfungwa analia wakati akitafuta picha yake katika hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya 1996 ambayo karibu wafungwa 1,200 walipigwa risasi na walinzi wao. (faili)

UN yateua jopo kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu Libya

Haki za binadamu

Juhudi zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa za kushughulikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Libya leo zimepigwa keki na uteuzi wa wachunguzi huru watatu kwenda kuorodhesha ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika kwenye taifa hilo la Afrika lililoghubikwa na vita.

Wakati hali ya usalama ikiendelea kuzorota na kukosekana kwa mfumo wa haki nchini Libya kumemfanya Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu (OHCHR) Michelle Bachelet kumteua Mohamed Auajjar kutoka Morocco, Tracy Robinson kutoka Jamaica na Chaloka Beyani kutoka Zambia na Uingereza ili kuendesha uchunguzi huru. 

Bi. Bachelet amesema “Jopo hili la wataalam litatumika na mfumo wa kushughulikia ipasavyo hali ya kuenea kwa ukwepaji sheria kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na utekelelezaji wa ukatili mwingine na pia kutumika kama silaha ya kuzuia ukiukwaji zaidi na kuchangia katika amani na utulivu wan chi hiyo.” 

Mazingira ya ukwepaji sheria 

Mkuu huyo wa haki za binadamu ametaja kwamba mauaji , utesaji, ukatili wa kingono unaohusiana na machafuko, utekaji, watu kutoweshwa na ukatili katika mitandao ya kijamii vinaendelea katika mazingira ya ukwepaji sheria. 

Mbali ya hayo amesema watetezi wa haki za binadamu , wanaharakati na waandishi wa Habari wamekuwa wakishambuliwa na kulazimishwa kuikimbia nchi yao. 

Jopo hilo la kusaka ukweli nchini Libya limeundwa na Baraza la haki za binadamu tarehe 22 Juni 2020 ili Pamoja na mambo mengine liorodheshe madai yote ya ukiukwaji na ukatili wa haki za kimataifa za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu unaofanywa na pande zote nchini Libya tangu mwanzoni mwa mwaka 2016. 

Hali inazidi kudorora Libya 

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikiitupia jicho Libya kila wakati na Baraza la Usalama tangu kuangushwa kwa utawala wa dikteta wa zamani Muammar Gaddafi. 

Mwezi Juni Katibu Mkuu Antonio Guterres alielezea kushitushwa san ana kubainika kwa makaburi ya Pamoja nchini Libya na mwezi Julai akaliambia Baraza kwamba zaidi ya watu 400,000 wametawanywa na machafuko nchini humo. 

Na kati ya Aprili Mosi na Juni 30 mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL uliorodhesha takriban vifo 102 vya rai ana wengien54 waliojeruhiwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 172 ukilinganisha na miezi mitatu yam waka 2020. 

Wakati huohuo shirika la afya duniani WHO limeorodhesha takriban mashambulizi 21 dhidi ya vutuo vya afya, magari ya kubeba wagonjwa na wahudumu wa afya. 

Matokeo 

Mwezi ujao tume huru ya uchunguzi itatoa taarifa yam domo kwenye Baraza la haki za binadamu ya matokeo ya walichoshuhudia. 

Na mwaka 2021 wataalam hao wataandika ripoti ya kina kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Libya ikiwemo katika juhudi za kuzuia na uhakikisha uwajibikaji kwa ukiukwaji na ukatili wa haki za binadamu, Pamoja na mapendekezo ya kusonga mbele.