Kampeni za chanjo a polio zaanza tena Afghanistan na Pakistan baada ya COVID-19 kuwakosesha chanjo watoto milioni 50  

11 Agosti 2020

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo mjini Kathmandu, Nepal na shirika la kuhudumia watoto UNICEF, kampeni za chanjo ya polio zimeanza nchini Afghanistan na Pakistan, nchi mbili za mwisho kuwa na ugonjwa wa polio duniani.  

Kampeni ya pili ya chanjo ambayo itaenda karibia nusu ya nchi nzima inaanza mwezi huu baada ya ile iliyofanyika katika majimbo matatu mwezi Julai na kuwafikia takribani watoto 780,000.  

Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Asia Kusini, Jean Gough amesema, “chanjo hizi za kuokoa maisha ni muhimu kwa watoto ikiwa watoto wanatakiwa kuepuka janga lingine la afya. Kama ambavyo dunia imejionea vizuri, virusi havina mipaka na hakuna mtoto yuko salama kwa polio hadi kila mtoto awe salama.” 

Polio ugonjwa unaoambukiza sana,ugonjwa mbaya unaoweza kuepukwa kwa kwa chanjo. Watoto wa chini ya umri wa mika amitano wako katika hatari zaidi.   

UNICEF inasema matumizi ya miongozo mipya ya chanjo na matumizi ya vifaa vipya vya kujikinga vinavyotumiwa na wahudumu wa afya walioko mstari wa mbele vitasaidia kuhakikisha kampeni ya chanjo inaanza kwa usalama.  

Ingawa kila juhudi zitafanywa ili kuwafikia watoto kote katika nchi hizo mbili, UNICEF ina wasiwasi kuwa huenda watoto takribani milioni moja nchini Afghanistan wanaweza kukosa chanjo kwa kuwa chanjo ya nyumba kwa nyumba haiwezekani katika baadhi ya maeneo na wazazi watalazimika kwenda katika kiliniki za afya ili watoto wao waweze kuchanjwa. Nchini Paksitani nako, kusimamishwa kwa chanjo kumesababisha kuanza na kuongezeka kwa ugonjwa huo katika maeneo mapya nchini humo.  

 “Ingawa tumepata changamoto mpya jatika kupambana na polio kwasababu ya COVID-19, utokomezaji wa ugonjwa huu wa kuambukiza utarejea katika mstari, na uko katika uwezo wetu.” Amesema Jean Gough.  

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter