Mchango wa vijana kuleta mabadiliko Tanzania ni mkubwa:Restless Development

Abel Koka kutoka Restless Development Iringa nchini Tanzania katika mahojianon na Idhaa ya Kiswahili.
UN News/Grece Kaneiya
Abel Koka kutoka Restless Development Iringa nchini Tanzania katika mahojianon na Idhaa ya Kiswahili.

Mchango wa vijana kuleta mabadiliko Tanzania ni mkubwa:Restless Development

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika kuelekea siku ya vijana duniani itakayoadhimishwa 12 Agosti juma hili ni bayana kwamba vijana kila kona bado wanakabiliwa na changamoto lukuki na mara nyingi mchango wao wa kuleta mabadiliko ama hauonekani au unapuuzwa, lakini sasa hatua zinachukuliwa kubadili hali hiyo ikiwemo nchini Tanzania. 

Kama ilivyo kwingineko Tanzania nako hali imekuwa hivyo kwa muda mrefu, lakini sasa mambo yanabadilika kwani kupitia mchango wa mradi wa mafunzo kwa vijana yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Restless Development nchini humo vijana wanadhihirisha uwezo wao wa kuleta mabadiliko katika jamii na kutatua changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya ya uzazi na ujasiriamali. 

Amani Makalani mwenye umri wa miaka 24 kutoka mkoani Iringa Tanzania ni miongoni mwa vijana hao ambaye alijiunga na Restless Development kupitia mitandao ya vijana na kwa mafunzo aliyopata amekuwa akijitolea kufundisha viajana katika shule mbalimbali kuhusu kujitambua, elimu ya jinsia na kuwaandaa kuwa viongozi 

Tunawafundisha vijana kuhusiana na uongozi ambapo kijana ataweza kufahamu kiongozi ni nani na kiongozi ana sifa zipi na kiongozi afanye nini na kwa wakati gani tunafurahi sana kuona mapokeo ya wanafunzi jinsi tunavyowafundisha naama ambayo sisi tunatumia kufundisha Restless Development ni maana tofauti kama wanavyofundisha katika masomo ya kawaida.Tunatumia kamba ,nyimbo na mitindo mbalimbali ambayo inafanya wanafunzi waweze kuelewa kwa urahisi.Lakini pia huwa tunakaa na  mwanafunzi mmoja mmoja kwa kuweza kuongea nao na kufahamu matatizo yao na kuwashauri pia ilikuweza kufikia malengo yao

Mbali ya utoaji elimu kwa vijana Amani ameweza pia kuwa mjasiriamali wa kutengeneza sababu na kuweza kuanzisha miradi yake binafsi. Lakini si peke yake anayeshamiri kupitia Restless Development , jijini Dar Es Salaam tunakutana na Hawa Sindika mkufunzi wa biashara na stadi za maisha Kwa mimi binafsi nimeweza kufungua kampuni yangu inaitwa sacure community ambayo tuliweza kupata fursa ya  kwenda kufanya mafunzo ya biashara na stadi za maisha  mkoani indindi .Huko tukakutana na fursa nzuri ya kuuza nazi hapa  Dar es Salaam tukaweza kuuza nazi kwa wateja wengi ambapo tumeweza kufahamika zaidi.Tulipoona inakuwa tunaona kwanini tusiweze kuiongezea dhamani biashara yetu na hapo ndio tukaanza kununua mashine za kukuna nazi ilituweze kupata wateja wengi zaidi.Hapa ndipo kupitia hii mashine moja tuliyo inunua tuliweza kununua mashine nyingi zaidi ambazo tumeziweka kwenye masoko mbalimbali  hapa Dar es Salaam. Tumeweza kuajiri vijana sita kwenye masoko mbalimbali kufikia hii biashara mimi nimeweza kununua kiwanja changu na kuweza kujenga nyumba yangu mwenyewe 

Vijana hawa ni sehemu ndohgo tu ya mamia ya vijana ambao sasa wanajitambua na kusaidia vijana wenzao katika jamii kupitia mradi wa mafunzo wa Restless Development Tanzania.