Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi afariki dunia baada ya kuambukizwa COVID-19, Uganda

Martha Achok akikuza uelewa kuhusu jinsi ya kuzuia kusambaa kwa COVID-19 nchini Uganda.
UN Women /Aidah Nanyonjo
Martha Achok akikuza uelewa kuhusu jinsi ya kuzuia kusambaa kwa COVID-19 nchini Uganda.

Mkimbizi afariki dunia baada ya kuambukizwa COVID-19, Uganda

Afya

Shirka la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda limesikitishwa na kifo cha kwanza kabisa cha mkimbizi kutokana na virusi vya corona au COVID-19 tangu mlipuko wake utangazwe nchini humo mnamo Machi mwaka huu.

Kifo chake kimeripotiwa wakati vifo na visa vya mambukizi vinaongezeka kila uchao nchini humo. Hii hapa maelezo zaidi na John Kibego, mwandishi wetu kutoka Uganda.

Katika taarifa iliotolewa na UNHCR adhuhuri ya leo, marehemu ni kijana mkimbizi mwenye umri wa miaka 26 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Amekuwa akiishi katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Kikuube magharibi mwa nchi.

Kulingana na Roco Nuri, afisa wa mawasilaino wa UNHCR Uganda, mkimbizi huyo alipata pumzi ya mwisho hapo tarehe 8 mwezi huu wa Agosti akitunzwa kwenye hospitali ya rufaa ya Hoima, alikolazwa baada ya kuonesha dalili za virusi vya corona.

Ameongeza kuwa wanashirikiana na maafisa wa afya wa serikali na wadau wengine kutafuta watu wanoshukiwa kugusana na marehemi kambini humo na tayari zaidi ya 30 wamebainika na kuwekwa katika karantini ya kitaasisi katika kambi hiyo.

Bwana nuri ameonya kuwa kifo hiki ni kumbusho kuwa mlipuko wa COVID-19 ni janga la kimataifa linaloweza kuathiri yeyote bila kubagwa.

Na kuongeza kuwa wakimbizi nwamesalia miongoni mwa vikundi vilivyohatarini na vyenye fursa ndogo za kuhimili atahri za kiuchumi na kijamii za COVIDI-19 hususani watu wneye ulemavu wazee, watoto na wanawake.

Hata hivyo Nuri amesema wameimarisha uhamasishaji wa jamii kuhusu COVID-19 ili kuzuia mambukizi na vifo zaidi vinavyoweza kuongezeka katika jamii hiyo.

Dkt. Nicholas Kwikiriza Magambo, afisa wa afya wa wilaya ya Kikuube amesema wanachunguza madai kuwa marehemi alisafiri kwenda DRC na kurejea kambini kivyake hivi karibuni ambacho kitawasaidia kubaini chanzo cha mlipuko wa corona kambini.

Mkimbizi huyo amekuwa ni mtu wa nane kufariki dunia na kufikisha jumla ya mambukizo hadi 1,283 wakiwemo 1,115 waliopona.

Uganda ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya milioni moja na laki nne.