Waathirika wa homa ya ini aina B wamepungua 2019:WHO
Waathirika wa homa ya ini aina B wamepungua 2019:WHO
Kiwango wa watoto wa chini ya miaka mitano wanaougua homa ya ini aina B kilishuka mwaka 2019 hadi chini ya asilimia 1 kutoka asilimia 5 katika miaka 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
Kupitia taarifa ya makadirio iliyotolewa leo na WHO kuelekea siku ya homa ya ini duniani hapo kesho Julai 28, haya ni moja ya mafanikio makubwa ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs, ya kupunguza maambukizi hadi chini ya asilimia 1 kwa watoto wa umri wa chini ya miaka 5 ifikapo mwaka 2020.
Akizungumzia umuhimu wa juhudi za kutokomeza homa hiyo inayoenezwa na virusi mkurugenzi mkuu wa WHO Dk.Tedross Adhamon Ghebreyesus amesema “Hakuna mtoto anayestahili kuzaliwa kukua na kisha kufa na homa ya ini aina ya B kisa? hakupatiwa chanjo. Mafanikio ya leo ya kihistoria yanamaanisha kwamba tumepunguza kwa kiasi kikubwa visa vya magonjwa ya ini na saratani ya ini katika vizazi vijavyo. Kuzuia maambukizi ya homa ya ini aina B kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni mkakati muhimu sana wa kukabiliana na ugonjwa huo na kuokoa maisha. Hata wakati huu wa janga la corona au COVID-19 ni lazima tuhakikishe kwamba kina mama na watoto wachanga wana fursa ya huduma za kuokoa maisha ikiwemo chanjo ya homa ya ini aina B.”
Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa. Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.Katika siku ya homa ya ini duniani mwaka huu 2020 WHO inatoa wito kushirikiana na kuchukua hatua kuendeleza mafanikio haya kupitia juhudi za kuzuia maambukizi ya homa hiyo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kwa kufanya vipimo kwa kina kwa kina mama wajawazito na kuwapa dawa za kuzuia homa hiyo kwa wanaohitaji , lakini pia kuhakikisha huduma ya chanjo ya homa ya ini aina ya B inapatikana kwa watoto wachanga.
Duniani kote shirika hilo linasema watu milioni 250 wanaishi na homa sugu ya ini aina B na inakatili maisha ya watu 900,000 kila mwaka wakiwemo watoto.