Ndoto za watoto kuwa marubani Tanzania, sasa zaanza kutimia

14 Julai 2020

Nchini Tanzania, taasisi ya kijamii ya Tanzania Youth Aviation, yenye lengo la kuhamasisha vijana na watoto kuingia katika faniya urubani na uongozaji wa ndege imeanza kufanikiwa katika kufikia lengo lake hilo wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa na wadau wanataka wasichana nao wajiunge na masomo ya sayansi, teknolojia  na hisabati, STEM. 

Tanzania Youth Aviation foundation yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam katika taifa hili la Afrika MAshariki alianza kazi yake mwaka 2017 na kupata usajili rasmi mwaka 2019 ambapo mwenyekiti wake John Kamuli ametueleza kuwa, “siku za nyuma hata sasa ilionekana kwamba tasnia ya usafiri wa anga ni sekta ambayo imejificha ni familia tu baadhi zinaweza kufahamu. Mfano kama wewe, baba yako ni rubani unaweza kufahamu kuwa pengine kuna hivi, au kama anafanya kazi uwanja wa ndege utakuwa unajua. Lakini sasa wale vijana ambao wana ndoto hizo kwenye malengo yao ya maisha, namna ya kufika ilikuwa ni vigumu sana. Kwa hiyo ndio maana tukaanzisha hii taasisi kwa ajili ya kuweza kuwafikia wale vijana.”

Tulimuuliza Bwana Kamuli hadi sasa ni jambo gani wamefanya kufikia lengo la kuanzisha taasisi hiyo ambapo amesema kuwa, “tunacho kitengo ndani ya hii programu yetu inaitwa Youth Aviation Awareness Programe ambayo ndani yake ina vitu vingi, mfano Future indomitable aviators, hii unaona inaendesha kundi la Whatsapp wakati wanafunzi wakiwa likizo kwa ajili ya kuwaunda.”

Miongoni mwa wanufaika wa taasisi hii ya TYAF ni Matilda Mosem Mashauri ambaye anasema kuwa, “kuwa katika hii taasisi najisikia vizuri na faraja, kwa kuwa inaweza kuniongoza kunifikisha katika ndoto zangu za malengo ya kuwa katika tasnia ya anga. Vile vile nawakaribisha vijana wengine waje wajiunge nasi siyo lazima uwe rubani, bali kuna mambo mengi kwenye tasnia ya anga kama vile uhandisi, uanasheria wa masuala ya anga na kadhalika.’

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter