Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wanaokabiliwa na njaa duniani wanaendelea kuongezeka:Ripoti ya UN

Mradi wa FAO wa uhakika wa chakula (PESA) katika sekta ya kilimo, mifugo, maendeleo vijijini, uvuvi na kilimo
© FAO-Magnum Photos/Alex Webb
Mradi wa FAO wa uhakika wa chakula (PESA) katika sekta ya kilimo, mifugo, maendeleo vijijini, uvuvi na kilimo

Watu wanaokabiliwa na njaa duniani wanaendelea kuongezeka:Ripoti ya UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani inaendelea kuongezeka kwa imesema ripoti mpya ya hali ya uhakika wa chakula na lishe duniani iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa ruipoti hiyo ya pamoja ya mwaka 2020 iliyotolewa mjini Roma Italia na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo FAO na la afya duniani WHO, ingawa hali ni mbaya na ya kukatisha tamaa lakini bado kuna matumaini ya kufikia lengo namba mbili la maendeleo endelevu au SDGs la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030 endapo hatua madhubuti zitachukuliwa sasa , la sivyo lengo halitofikiwa mwaka 2030 na mamilioni zaidi ya watu watatumbukia kwenye njaa na umasikini.

Niger inakumbana na upungufu wa chakula na viwango vya mapato ya chini
WFP/Simon Pierre Diouf
Niger inakumbana na upungufu wa chakula na viwango vya mapato ya chini

Mkurugenzi mkuu msaidizi na mchumi mkuu wa FAO Maximo Toredo akifafanua hali halisi ya uhakika wa chakula duniani amesema“Mwaka 2019 kumekuwa na watu karibu milioni 700 waliokabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula sawa na mtu 1 kati ya 10 na hii inamaanisha kwamba hatupigi hatua katika kupunguza lishe duni dumiani. Tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyumma tonaongezeko dogo badala ya idadi kushuka.”

Hilo limeungwa mkono na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye ameonya kwamba mwaka huu hali itakuwa mbaya zaidi kutokana na janga la corona "Janga la COVID-19 linafanya hali kuwa mbaya zaidi, watu wengi watatumbukia katika njaa mwaka huu, hatuwezi kuruhusu hili kutokea. Ripoti iko wazi endapo mwenendo wa sasa utaendelea hatutaweza kutimiza lengo la maendeleo namba 2 la kutokomeza njaa ifikapo 2030. Mabadiliko yanapaswa kuanza sasa.”

Umoja wa Mataifa na harakati za kusaidia kuhakikisha uhakika wa chakula.
IFAD/GMB Akash
Umoja wa Mataifa na harakati za kusaidia kuhakikisha uhakika wa chakula.

Tathimini ya awali ya ripoti hiyo inasema  janga la COVID-19 liaongeza kati ya watu milioni 83 na milioni 132 kwenye jumla ya watu wenye lishe duniani duniani kwa mwaka 2020. Toredo  anasema huu ni mtihani kubwa "Hii inamaanisha kwamba hatua zozote zilizopigwa kwa mfano katika kupunguza umasikini kwa miaka 10 iliyopita zimepunguzwa na suala la lishe dunia ambalo limekuwa likiongezeka katika miaka iliyopita hali itakuwa mbaya zaidi kwa ongezeko kubwa la watu wenye njaa na maana yake ni kwamba itakuwa  vigumu zaidi kufikia lengo namba 2.”

Ripoti imependekeza kwamba ili kufikia lengo namba mbili mwaka 2030 ni lazima gharama ya lishe bora dunini zipungue ili kuwezesha watu wengi zaidi kuweze kumudu lakini pia kuwe na mikakati thabiti ya kupunguza idadi ya watu wasio na uhakika wa chakula kwa kuwajengea uwezo wazalishaji na wasambazaji wa chakula duniani.