Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatangaza jopo huru la kutathimini mapambano dhidi ya COVID-19 dunini

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19
UN Photo/Evan Schneider
Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza katika moja ya taarifa za WHo kuhudsu janga la COVID-19

WHO yatangaza jopo huru la kutathimini mapambano dhidi ya COVID-19 dunini

Afya

Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO Alhamisi wiki hii ametangaza kuundwa kwa jopo huru (IPPR) kwa ajili ya maandalizi na hatua zilizochukuliwa kukabiliana na janga la corona au COVID-19 duniani.

Katika taarifa yake kwa nchi wanachama wa WHO mkurugenzi huyo Dkt. Tedros Adhamon Ghebreyesus amesema kazi kubwa ya jopo hilo itakuwa ni kutathimini hatua za kimataifa za kukabiliana na janga la COVID-19.

Ameongeza kuwa jopo hilo litakuwa na wenyeviti wenza wawili ambao ni waziri mkuu wa zamani wa New Zealand Helen Clack na Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf.

Mbali ya kuwa waziri mkuu wa New Zealand Helen Clack aliteuliwa kuliongoza shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Rais Sirleaf ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel.

Dkt. Tedross amesema jopo hilo huru ambalo litakuwa na mwaka mzima wa kufanya kazi yake wenyeviti watachagua wajumbe wengine wa jopo hilo na pia wajumbe wa secretariat huru ambayo itawasaidia kutekeleza majukumu yao.