Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Covid-19 inabadili hatua zilizopigwa kutokomeza umasikini, katika afya na elimu:UN

Wanawake na wasichana wakibeba maji huko Nigeria
World Bank
Wanawake na wasichana wakibeba maji huko Nigeria

Covid-19 inabadili hatua zilizopigwa kutokomeza umasikini, katika afya na elimu:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Juhudi za kimataifa zilizozinduliwa mwaka 2015 kuboresha Maisha ya watu kote duniani kupitia ufikiaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu au SDGs ifikapo mwaka 2030, zimeathirika vibaya na janga la virusi vya corona au COVID-19 kwa mujibu wa makadirio ya ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo Jumanne.

Akizungumza katika mjadala wa ngazi ya juu wa utoji wa ripoti hiyo kupitia mtandao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Wakati nchi wanachama walibaini kwenye mkutano wa kimataifa wa SDG’s Septemba mwaka jana, juhudi za kimataifa kufikia leo hazitoshi kuleta mabadiliko tunayoyahitaji, na hivyo kuweka njiapanda ahadi ya ajenda ya maendeleo kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavyo. Sasa kutokana na COVID-19 mgogoro wa kiafya, kiuchumi na kijamii unatishia maisha ya watu na uwezo wao wa kujikimu na kufanya ufikiaji wa SDGs kuwa mgumu zaidi.”

Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya masuala ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa (DESA) inathibitisha kwamba juhudi za kimataifa za kufikia malengo 17 ya SDG’s ifikapo mwaka 2030 ytayari zilikuwa ziko nyuma mwishoni mwa mwaka 2019 hata kabla ya janga la corona na sasa janga hilo la COVID-19 limezusha tafrani kubwa katika kipindi kifupi na kusababisha kuingilia hatua za ufikiaji wa SDGs na kuwaacha watu walio hatarini zaidi na nchi masikini kuathirika zaidi.

Ufikiaji SDGs unasuasua

Hayo yameungwa mkono na Katibu Mkuu Guterres ambaye amesisitiza kwamba Hata kama virusi vya corona vinamuathiri kila mtu na kila jamii lakini sio kwa viwango sawa, bali vimeanika na kuongeza pengo la haki na usawa lililokuwepo.

QUOTE: “Hata kama virusi vya corona vinamuathiri kila mt una kila jamii lakini sio kwa viwango sawa-Antonio Guterres”

Kwa mujibu wa ripoti ya hatua zilizopigwa kwenye SDGs ya mwaka 2020 , dunia ilikuwa inapiga hatua ingawa zisizolingana kila mahali na zisizotosheleza kutimiza malengo hayo kwenye maeneo kama kuboresha huduma za afya za mama na mtoto, kupanua wigo wa huduma ya nishati ya umeme na kuongeza idadi ya uwakilishi wa wanawake katika serikali.

Ripoti inasema hata hivyo hatua hizo zimeathiriwa na kutokuwepo kwa uhakika wa chakula, uharibifu wa mazingira na kuendelea kwa pengo la usawa.

Leo hii kwa mujibu wa ripoti janga la COVID-19 limekuwa mgogoro mbaya zaidi wa kiuchumi na kibinadamu katika kizazi hili, likisambaa katika nchi zote na kusababisha vifi Zaidi ya 500,000 na wagonjwa zaidi ya milioni 10 waliothibitishwa.

Kwa kutumia takwimu na makadirio ya karibuni kabisa ripoti hiyo yam waka hya hatua za ufikiaji SDGs inaonyesha kwamba watu masikizi kabisa na walsiojiweza wakiwemo watoto, wazee na watu wenye ulemavu, wahamiaji na wakimbizi ndio walioathirika Zaidi na athari za COVID-19. Imeongeza kuwa wanawake nao ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa janga hilo.

Matokeo ya ripoti

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya DESA watu milioni 71 wanatarajiwa kutumbukia katika umasikini uliokithiri mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la kwanza kubwa katika umasikini duniani tangu mwaka 1998.

Kupotea kwa kipato, ukosefu wa ulinzi wa hifadhi ya jamii na kupanda kwa bei kunamaanisha kwamba hata wale ambao awali walikuwa wanajiweza sasa watajikuta katika tishio kubwa la umasikini na njaa.

Lengo nambari moja la malengo ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza  umaskini na njaa
World Bank/Jamie Martin
Lengo nambari moja la malengo ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza umaskini na njaa

Kiwango kidogo cha ajira na kukosekana kabisa kwa ajira kutokana na COVID-19 inamaanisha kwamba watu bilioni 1.6 ambao tayari ni wafanyakazi walio katika hali tete katika sekta zisizorasmi, nusu ya nguvu kazi yote duniani wanaweza kuathirika vibaya inasema ripoti.

Pato lao tayari limeshuka kwa asilimia 60 katika mwezi wa kwanza wa janga hili.

Matokeo mengine ya ripoti hiyo ni kwamba zaidi ya wakazi bilioni moja wa mitaa ya mabanda kote duniani wako katika tishio kubwa la athari za COVID-19, wakiathirika kwanza na makazi duni, kukosa huduma za maji nyumbani, kutumia choo kimoja wakiwa wengi kuwa na mifumo michache ya maji taka au kutokuwa nayo kabisa, kufurika kwa usafiri wa umma na fursa finyu ya vituo rasmi vya afya.

Waandishi wa ripoti hiyo wanakadiria kwamba wanawake na Watoto ni miongoni mwa waathirika wakubwa kutokana na janga hilo. 

Imeongeza kuwa kuvurugwa kwa huduma za afya kama utoaji chanjo na fursa ndogo ya kupata chakula na lishe vinaweza kusababisha ongezeko la maelfu kwa maelfu ya vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka 5 na maelfu ya vifo vya kina mama wakati wa kujifungua kwa mwaka huu wa 2020. 

Pia nchi nyingi zimeshuhudia ongezeko la ukatili majumbani dhidi ya wanawake na watoto.