Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 na mabadiliko ya tabia nchi vimeonesha wazi hitaji la kuimarisha ushirika na mshikamano

Umoja wa Mataifa unakumbuka kuwa vyama vya ushirika ni sehemu ya suluhisho la ukosefu wa usawa.Mkulima wa mananasi kutoka Argentina. Ingawa mananasi hayo yanasambazwa maeneo mbalimbali duniain bado hali za wakulima zinasalia duni.
UNDP Green Commodities Programme
Umoja wa Mataifa unakumbuka kuwa vyama vya ushirika ni sehemu ya suluhisho la ukosefu wa usawa.Mkulima wa mananasi kutoka Argentina. Ingawa mananasi hayo yanasambazwa maeneo mbalimbali duniain bado hali za wakulima zinasalia duni.

COVID-19 na mabadiliko ya tabia nchi vimeonesha wazi hitaji la kuimarisha ushirika na mshikamano

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Janga la COVID-19 na dharura ya tabianchi, vyote viwili vimefunua udhaifu wa jamii zetu na sayari yetu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kuhusu siku ya vyama vya ushirika inayoadhimishwa kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi Julai.

Bwana Guterres akifafanua kuhusu hilo amesema majanga hayo mawili yanaathiri vibaya nchi na watu walio katika mazingira magumu zaidi ulimwenguni na hali hiyo inaimarisha mizozo mingi ya kijamii na kiuchumi. Pia matatizo hayo yanaonesha wazi hitaji la kuimarisha ushirikiano na mshikamano wa kimataifa.

“Maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya kimataifa vyama vya ushirika yanaangazia mchango ambao vyama vya ushirika vinatoa katika kushughulikia changamoto hizi, kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu,SDGs na kuunda njia ya kuelekea siku zijazo za ujumuishaji na usawa.” Amesema Guterres katika ujumbe wake.

Aidha Katibu Mkuu Guterres amesema, vikiwa vimewekwa katika kanuni za utunzaji jamii, kujitawala kidemokrasia, kukuza ajira na ulinzi wa mazingira, vyama vya ushirika vimewekwa vizuri kusaidia kuharakisha hatua kwenye ahadi walizojiwekea wanadamu.

“Vyama vya ushirika na biashara zingine za uchumi na mshikamano pia zinaweza kuelekeza njia kuelekea mnepo wakati wa shida. Siku hii ya Kimataifa itumike kama ukumbusho wa jukumu muhimu la vyama vya ushirika katika kukuza mshikamano wakati huu wa jaribio la kushangaza kwa familia ya binadamu. ”Amesisitiza Bwana Guterres.