Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yapata wasiwasi kuhusu maandamano ya Ethiopia, yasihi uchunguzi wa kina kuhusu kuuawa kwa Hachalu Hundessa

Wahamiaji kutoka Ethiopia waliokuwa wamekwama nchini Yeman wakirejea Addis Ababa kwa msaada wa IOM (Julai 2019)
IOM Bole Addis Ababa International Airport
Wahamiaji kutoka Ethiopia waliokuwa wamekwama nchini Yeman wakirejea Addis Ababa kwa msaada wa IOM (Julai 2019)

OHCHR yapata wasiwasi kuhusu maandamano ya Ethiopia, yasihi uchunguzi wa kina kuhusu kuuawa kwa Hachalu Hundessa

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR kupitia taarifa yake iliyoitoa leo Julai 3 mjini Geneva Uswisi, imeeleza kusikitishwa sana na matukio ya vurugu nchini Ethiopia ambako mwibaji maarufu na mwanaharakati kutoka katika eneo la Oromia, Hachalu Hundessa alipigwa risasi na kuuawa jumatatu katika mji mkuu Addis Ababa

Kuuawa kwa Hundessa kumechochea maandamano nchi nzima ukiwemo mji mkuu na pia katika mkoa wa Oromia. Wakati baadhi ya maandamano yalikuwa ya amani, mengin mengine yalikuwa ya vurugu tangu mwanzo.

Taarifa ya OHCHR imesema, “kwa mujibu wa taarifa tulizozipokea, barabara ziliripotiwa kufungwa katrika maeneo mengi ya mkoa wa Oromia na pia majengo kuvamiwa na kuchomwa moto, wakati huo huo kulikuwa na milipuko ya risasi na mabomu katika mji mkuu Addis Ababa."

Mamlaka za Ethiopia zilichukua hatua ya kuzuia kuenea kwa maandamano kwa kufunga mtandao wa intaneti ktika mkoa wa Oromia na pia mjini Addis Ababa na hivyo kufanya kuwa vigumu kuweza kuthibitisha ripoti kuhusu idadi ya watu waliouawa na wale waliojeruhiwa. Kwa mujibu wa serikali, takribani watu hamsini waliuawa, lakini kwa mujibu wa vyanzo vya vyombo vya habari, inaonekana takribni watu 80 wamefariki dunia wakiwemo wattu kutoka vikosi vya usalama.

“Tunatambua kwamba maandamano yaliyofuatia mauaji ya Hundessa yamezidi kuongezeka kwa misingi ya kabila. Kwa hivyo tunatoa wito kwa wote, ikiwa ni pamoja na vijana, kuacha kufanya mashambulizi ambayo yana misingi ya kikabila na pia kuacha kuchochea vurugu,  vitendo ambavyo vinazidisha mvutano.Aidha tunatoa wito kwa vikosi vya usalama kutotumia nguvu isiyo ya lazima au isiyo na mipaka.” Imetoa wito ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

 Watu 35 wanaripotiwa kuwa wamekamatwa na vikosi vya usalama Jumanne jioni wakati wa maandamano kuhusina nae neo la kumzika Hundessa. Kwa mujibu wa polisi, waandamanaji waliokuwa wanataka Hundessa azikwe Addis Ababa, walijaribu kuzuia mwili wa mwanamuziki huyo usipelekwe katika mji wa Ambo alikozaliwa, lakini hatiumaye maziko yalifanyika katika mji huo siku ya Alhamis.

Mamlaka za Ethiopia zinasema zimeshamkamata mtu anayetuhumiwa kumuua Hachalu Hundessa lakini pia ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa ni muhimu uchunguzi wa kina na ulio huru ufanyike kwa uwazoi kuhusu mauaji haya ili wale wanaohusika wafikishwe katika mikono ya sheria.

“Pia tuko tayari kuisaidia tume ya haki za binadamu ya Ethiopia katika kuchunguza uwezekano wa ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa matukio haya ya vurugu.” Imesema OHCHR.