Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujasiriamali waweza kuwa suluhu ya ajira kwa vijana baada ya COVID-19:UN

Ellen Chilemba, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tiwale, shirika linaloongozwa na vijana nchini Malawi.
Tiwale
Ellen Chilemba, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tiwale, shirika linaloongozwa na vijana nchini Malawi.

Ujasiriamali waweza kuwa suluhu ya ajira kwa vijana baada ya COVID-19:UN

Ukuaji wa Kiuchumi

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa imebaini kwamba ujasiriamali unaweza kuwa suluhu kubwa ya ajira kwa vijana na kusaidia jamii nyingi zisizojiweza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa mjini New York na idara ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) , kuondoa vikwazo ambavyo vinawazuia vijana kuwa wajariliamali wenye mafanikio kutachangia kwa kiasi kikubwa kusonesha mbele maendeleo endelevu na kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19.

Ripoti hiyo ya dunia ya vijana kwa mwaka 2020 iliyopewa jina “Ujasiriamali wa kijamii kwa vijana na ajenda 2030” imetoa wito kwa serikali na wadau wengine wafanyamaamuzi “kuondoa vikwazo kwa ujasiriamali kwa vijana kama vile fursa ya kupata mitaji ya kuanzia ambayo kwa sasa ni adimu na inawazuia vijana wengine kujihusisha katika shughuli mbalimbali zinazoweza kuwaletea faida.”

Imeongeza kuwa mifumo mingi ya ufuatiliaji pia mara nyingi inakuwa kikwazo ama bila kujua inawakosesha vijana wengi kupata fursa za mikopo ya kifedha na huduma zinazohitajika kuanzisha shughuli za ujasiriliamali.

Na uhaba wa fursa za mafunzo, msaada wa kiufundi, mitandao na masoko vimeelezwa na ripoti hiyo kuwa ni sababu zingine zinazowakatisha tamaa vijana kuanzisha miradi.

Ujasiriliamali ni nini?

Ripoti hiyo ya 2020 imeelezea ujasiriamali kama ni biashara ambayo inazalisha faida huku pia ikileta athari nzuri katika jamii. Ripoti inasema biashara za ujasiriliamali katika jamii zimewanufaisha watu milioni 871 katika kipindi cha miezi tisa tu kwenye nchi za Ulaya na Asia ya Kati mwaka 2016, kwa kutoa huduma na bidhaa zenye gharama ya takriban dola bilioni 6.7 na kuunda ajira hususan kwa makundi ya watu waliotengwa hasa vijana.

Hakuna ukomo wa uanzishaji miradi ya ujasiriamali

Ripoti hiyo imeweka bayana kwamba vijana wajasiriamali  ambao tayari wameshaleta mabadiliko ni Pamoja na Zaid Souqi kutoka Jordan ambaye alianzisha ‘The Orenda Tribe” mwaka 2014 ambayo ni kazi ya Sanaa kwa ajili ya matumaini. Mradi wake wa Sanaa na mafunzo unawawezesha Watoto wa Syria na Jordan walio katika mazingira hatarishi.

Kila nchi inategemea vijana wake. Wakati vijana wanatetemeka, ulimwengu unadondoka. - Fatoumata Tamboura, miaka 15,mtoto  mwandishi wa habari. katika redio ya jamii  Kaoural FM  katika mkoa wa kati wa Mopti.
© UNICEF/Seyba Keïta
Kila nchi inategemea vijana wake. Wakati vijana wanatetemeka, ulimwengu unadondoka. - Fatoumata Tamboura, miaka 15,mtoto mwandishi wa habari. katika redio ya jamii Kaoural FM katika mkoa wa kati wa Mopti.

Mfano mwingine ni kutoka Malawi ambapo mkufunzi Ellen Chilemba alianzisha mradi wa Tiwale alipokuwa na umri wa miaka 18 na sasa ana miaka 30 mradi wake ni wa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali wanawake, na hadi kufikia sasa wameshatoa mafunzo ya ujasiriamali wanawake 150.

Na mradi mwingine ni Tyk ulioanzishwa na Al Rjula na washirika wake ambao lengo lake ni kuwapa utambulisho wa kuweza kujitawala kwa watu wasio na utaifa na wakimbizi.

Ukosefu wa ajira umewaathiri zaidi vijana

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ukosefu wa ajira miongoni mwa viajana bilioni 1.2 kote duniani uko juu zaidi ya watu wazima.

Janga la COVID-19 limeathiri Zaidi matarajio yao ya ajira na kusababisha vijana karibu milioni 25 zaidi kuingia kwenye kundi la wasio na ajira kote duniani.

Hata kabla ya janga la corona kuzuka huko Uchina Desemba 2019, na kabla ya kuwa janga la kimataifa  ripoti inasema wataalam wa masuala ya ajira walikadiria kwamba ajira milioni 600 zitahitajika katika miaka 15 ijayo ili kukidhi mahitaji ya ajira kwa vijana

Ikiainisha faida ambazo zinaweza kupatikana endapo serikali zimewekeza Zaidi kwa vijana wao ripoti hiyo imesema hatua mpya zingeweza kuchangia kusongesha mbele malengo ya amendeleo endelevu SDGs ambayo lengo lake ni kutokomeza umasikini hadi kuziba pengo la usawa.

“Kuweka njia kwa ajili ya ujasiriliamali kwa miradi ya vijana kunaweza kuleta matokeo chanya “ amesema Liu Zhenmin msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kiuchumi na kijamii na kuongeza kwamba “Wakisaidiwa kwa kuwezesha sera na program, ujasiriliamali unawasilisha njia bora kwa vijana kujipatia kipato , kuweza kuishi kwa kujitegemea na kuboresha ulimwengu unaowazunguka.”