Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yawaenzi wafanyakazi wake waliopoteza maisha kazini

Bendera ya Umoja wa Mataifa inapepea nusu kama ishara ya mshikamano na New York na kuwakumbuka waathiriwa wa mlipuko wa COVID-19 jijini hilo.
UN Photo/Evan Schneider
Bendera ya Umoja wa Mataifa inapepea nusu kama ishara ya mshikamano na New York na kuwakumbuka waathiriwa wa mlipuko wa COVID-19 jijini hilo.

UN yawaenzi wafanyakazi wake waliopoteza maisha kazini

Masuala ya UM

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliopoteza Maisha wakiwa kazini leo wameenziwa kwenye hafla maalum kwenye Umoja wa Mataifa kwa ushujaa wao na kwa huduma yao chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuokoa vizazi vijavyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “watu hao wamepoteza Maisha wakijaribu kumaliza kuanzia jinamizi la vita na kusaka viwango bora vya maisha na kuwa na uhuru kwa ajili ya wote .”

Ameongrza kuwa ukiwa mfanyakazi wa umoja wa Mataifa ni kawaida huko mashinani kukabiliana na hali tete kutokana na migogoro, vita na kutokuwepo utulivu na mwaka huu wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 75, janga la virisu vya corona au COVID-19 limezusha zahma isiyo ya kawaida.

Lakini Pamoja na hayo bado “Kote duniani hususan kwenye mazingira magumu Zaidi bendeya ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa ilionyesha matumaini . Kwamba tumaini ni sehemu ya waliotuachia wafanyakazi wenzutu tunaowaenzi leo. Walilipa gharama kubwa ya Maisha yao ili kwamba wengine wagange yajayo katika mustakbali bora.”

Kutoa ahadi

Katibu Mkuu amewaambia washiriki wa hafla hiyo kwamba anatambua bayana majukumu yake kwa wale waliopoteza maisha wakihudumu chini ya Umoja wa Mataifa, pamoja na familia zao na wapendwa wao na kwa wafanyakazi wote wa umoja wa Mataifa abao wanafanyakazi kweenye mazingira yasiyo salama nay a hatari ambako kifo kimoja ni vifo vingi.

Ameahidi “kuendelea kuhakikisha kwamba shirika letu wakati wote linatathimini na kuimarisha hatua zetu zinazohusiana na usalama na huduma kwa wafanyakazi. Wakati wafanyakazi wenzetu wanaolipa gharama kwa maisha yao ni wajibu wetu kuwaenzi na kuzisaidia familia zao.”

Kabla ya kuitisha ukimya wa dakika moja kwa ajili ya waliopoteza Maisha kati ya Machin a desemba mwaka 2019, amemtaka kila mtu “Kuenzi kumbukumbu za wenzetu waliopoteza Maisha kwa kuahidi kuchagiza amani, mafanikio na fursa kwa kila mtu , kila mahali kwa ajili ya vizazi vijavyo.”