Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tafakari kabla ya kueneza taarifa potofu ili kuzuia kusambaa kwa COVID-19:UN

Mara nyingine kueneza habari zozote zili kunaweza kuleta madhara mengi.
UN Social Media
Mara nyingine kueneza habari zozote zili kunaweza kuleta madhara mengi.

Tafakari kabla ya kueneza taarifa potofu ili kuzuia kusambaa kwa COVID-19:UN

Masuala ya UM

Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa watu kufanya maamuzi ya busara kwenye mitandao ya kijamii kama yale wanayyafanya katika kujitenga na mikusanyiko ili kuzuia kusambaa kwa janga la corona au COVID-19 na kuhakikisha wanatafakari kwa kina kabla ya kuweka au kusambaza taarifa mutandaoni.

Ujumbe huu ni wa karibuni kabisa kutoka kwenye mkakati wa Umoja wa Mataifa wa iliyothibitishwa au “Verified initiative” ambao unataka watu kote duniani kutafakari kabla ya kusambaza taarifa au maaudhi kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ya “tafakari kwanza” mkuu wa idara ya mawasiliano ya umaa wa Umoja wa Mataifa Melissa Fleming amesema “Moja ya njia ambazo taarifa potofu zinasambaa ni jinsi watu wanaosukumiana au kusambaziana kwenye motandao ya kijamii. Wazo la kusita na kutafakari kwanza ni kuhakikisha unatafakari kwanza kabla ya kusambaza taarifa. Ikianza kuwa hulka kwenye akili za watu na fikrika basi itawezesha watu kubadili tabia binafsi za kusambaza vitu mitandaoni.”

Kampeni hiyo ya sita au tafakari inajumuisha video, picha na zawadi za rangi za kuvutia na inasisitiza kwamba sambaza tu kwenye mitandao ya kijamii vitu ambavyo ni vya kuaminika na sahihi vyenye misingi ya kisayansi.

Kampeni hii ni ya kuwafanya watu watafakari kuhusu taarifa potofu ambazo mara nyingi zinachukuliwa kama “ni nzuri na za kuweza kusambazwa na zilizosheheni taarifa za wazi ambazo watu wanaowasiliana kwa makini na kutegemea masuala ya kisayansi hawawezi kuzisambaza kwa sababu hawataki kuanika kila kitu hadharani ameongeza Bi. Fleming

Akitoa mfano amesema mathalani tayari makundi ya wanaopinga chanjo yameshaanza kujitokeza na kusambaza taarifa za kupinga chanjo yoyote ya COVID-19 itsiku za usoni.

Nchi zilizoendelea kama Marekani, watoto wanaendelea na masomo kwa njia ya mtandao wakiwa nyumbani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona
© UNICEF/Lisa Adelson
Nchi zilizoendelea kama Marekani, watoto wanaendelea na masomo kwa njia ya mtandao wakiwa nyumbani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona

Mkakati wa iliyothibitishwa

Kupitia mkakati huu wa iliyothibitishwa, Umoja wa Mataifa umewaweka watu unaowaita “wahudumu wa kidijitali” ili kukabiliana na taarifa za uongo. Wahudumu hawa ambao ni zaidi ya 10,000 ambao wamejisajili kila siku na kila wiki kupokea taarifa mbalimbali kuanzia kuhakiki ukweli nchini Colombia hadi wanahabari chipukizi nchini Uingereza na idadi ya watu wanaojiunga inaongezeka kwa kiwango cha asilimia 10 kwa wiki kwa mujibu wa idara ya mawasiliano ya umaa (DGC).

Kampeni hiyo pia inaungwa mkono na nchi nyinge ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa. Kinara wa kampeni hiyo ikiwa nchi ya Lativia, theluthi mbili ya nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walitoa taarifa tarehe 12 Juni wakipinga vikli kusambaa kwa taarifa potofu zinazohusiana na COVID-19.

Taarifa yao ilisema “Tunatiwa wasiwasi kuhusu athari zinazosababishwa kwa makusudi na utoaji na usambazaji wa taarifa potofu au za kurubuni kuhusuiana na janga hili la COVID-19. Tunatoa wito wa kuchukua hatua kupambana na kuzagaa kwa taarifa potofu kwa njia bora na kwa kuheshimu uhuru wa raia wa kujieleza.”

Idadi kubwa ya makampuni ya Habari kote duniani pia yanasambaza taarifa za mkakati wa tafakari katika vyombo vyao vya Habari, mtandaoni na kupitia ujumbe wa simu za mkononi.

Lengo kubwa la kampeni hii ni kusaidia kuzuia kusambaa kwa taarifa potofu kuhusu COVID-19 kwenye mitandao ya kijamii amesema Bi. Fleming na kusisitiza kwamba mitandao kama Facebook au Twitter pekee ndio inayoweza kuzuia kusambaa kwa kasi taarifa potofu. Na kuongeza kuwa

“Pia tunahitaji jukwaa la kufanyakazi nasi. Umoja wa Mataifa unazungumza na makampuni hayo ya teknolojia . Majukwaa mengi ya mitandao ya kijamii yameahidi kuchagiza mkakati wa tafakari, huku yakiongeza juhudi zao za kukomesha kusambaa kwa taarifa za uongo.”