Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kukomesha ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana:Mohammed

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed (katikati), na msichana mdogo wakati wa ziara ya Djibouti katika Pembe la Afrika mnamo Oktoba 2019.
United Nations
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed (katikati), na msichana mdogo wakati wa ziara ya Djibouti katika Pembe la Afrika mnamo Oktoba 2019.

Ni wakati wa kukomesha ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana:Mohammed

Wanawake

Ni wakati wa kukomesha ukatili wa kijinsia unaowakabili wanawake,  wanaume na wavulana ni kitovu cha hili kote duniani kwa mujibu wa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed.

Kupitia ujumbe binafsi kuhusu jinamizi hilo la ukatili Bi. Mohammed amesema wanaume na wavulana ambao wanafumbia macho ukatili dhidi ya wanawake lazima wakubali kwamba wanashiriki ukatili huo.

Ameongeza kuwa wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19 Umoja wa Mataifa umeripoti ongezeko kubwa la ukatili majumbani wakati wanawake wengi wakilazimika kukwama na watu wanaowafanyia ukatili.

Hivyo ametoa wito kwa watu wote hususan kwa wanaume na wavula kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na kushikamana na wanawwake hao ambao ni mama zao, dada zao, binti zao na wenzi wao 

Wasichana wachanga katika kijiji cha Danja huko Niger wanashikilia ishara kuunga mkono mpango wa Spotlight wa Umoja wa Mataifa
UNFPA/Ollivier Girard
Wasichana wachanga katika kijiji cha Danja huko Niger wanashikilia ishara kuunga mkono mpango wa Spotlight wa Umoja wa Mataifa

 

“Duniani kote ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ikiwemo ubakaji unaongezeka. Matukio mengi yamechochea ghadhabu kubwa, lakini bado wengine wanajaribu kucheza mchezo wa zamani wa kupupa lawama kwa wengine. Wakilaumu janga la COVID-19, changamoto za kiuchumi na kijamii, hali ya sintofahamu, n ahata bila haya kuwalaumu waathirika, ambao mara nyingi ni wanawake au mbaya zaidi wasichana, nami nasema hakuna kingine chochote cha kulaumu isipokuwa watekelezaji “Katika ombi hilo Bi.Mohammed akaenda mbali zaidi na kusisitiza kwamba 

“Hebu na tuwe wazi, ukatili wa kingono na ukatili wa aina yoyote ile ni ukatili, na hakuna sababu juu ya hilo, hakuna kinachohalalisha  na tunapaswa kutouvumilia hata kidogo ukatili huo. Sisi sote ni lazima tusimame kidete na kuukemea”.

Naibu Katibu Mkuu huyo ambaye ni mama wa mabinti wanne hata hivyo amesema sauti iliyomsukuma kulipazia sauti suala hili ni ya watoto wake wa kiume .Akawageukia wanaume na wavulana na kuwaambia

“Wanaume na wavulana nazungumza nanyi, hili ni lenu, timizeni wajibu wenu, pazeni sauti, simameni na wanawake na wasichana, mjiunge na wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwa ajili ya amani kila mahali, katika maeneo ya vita na majumbani. Ungeni mkono mkakati wetu wa spotlight unaowataka wanaume kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.”