Nchi za Afrika zakutana kuimarisha utalii baada ya COVID-19:UNWTO

9 Juni 2020

Nchi 30 za Afrika zikiwaleta pamoja washiriki zaidi ya 140 wakiwemo mawaziri wa utalii na shirika la Umoja wa Mataifa la utalii duniani UNWTO, wamekutana kwa njia ya mtandao kujadili ukuzaji na mustakbali wa utalii endelevu barani humo.

Mada katika mkutano huo wa 63 ulioandaliwa na tume ya kanda ya Afrika ya shirika la utalii duniani (CAF) ni kujikwamua kutoka kwenye janga la corona na kujenga mnepo katika sekta ya utalii ukitathimini pia matukio mbalimbali makubwa yanayoikumba sekta hiyo kwa sasa.

Mbali ya mawaziri 24 wa utalii wa kanda nzima pia umejumuisha wawakilishia wa Muungano wa Afrika A, wawakilishi kutoka mataifa 10 ya kimataifa, mtandao wan chi zinazohusiana na UNWTO, Muungano wa masuala ya fedha wa mataifa ya Afrika Magharibi na sekta binafsi kwa lengo la kuwajumuisha Pamoja ili kuwa na seta imara na yenye nguvu ya utalii.

Vipaumbele vya kufufua utalii Afrika

Katika mkutano huo mbali ya kushughulikia changamoto za sasa zinazoletwa na janga la COVID-19 katika sekta ya utalii, majadiliano yao ymelenga pia katika masuala muhimu ya ajenda ya Afrika ya UNWTO, mkakati wenye lengo la kutoa muongozo katika sekta ya utalii katika masuala ya ukuaji endelevu kuelekea 2030.

Vipaumbele hivyo vinajumuisha “kuimarisha miundombinu ya utalii Afrika, kuboresha usafiri wa anga, kurahisisha upatikanaji wa visa, kuhakikisha usalama na usalama wa watalii, kuwekeza katika maendeleo ya wat una kuimarisha taswira kwingineko duniani.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter