Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti wa uvuvi ni muhimu ni wakati wa kutumia kila kona:FAO

Ukaguzi wa mara kwa mara unafanywa na walinzi wa pwani huko Lazio, Italia, ili kuhakikisha kuwa vyombo vya uvuvi vina leseni vizuri na kwamba vinalindwa vyema
FAO/Cristiano Minichiello
Ukaguzi wa mara kwa mara unafanywa na walinzi wa pwani huko Lazio, Italia, ili kuhakikisha kuwa vyombo vya uvuvi vina leseni vizuri na kwamba vinalindwa vyema

Udhibiti wa uvuvi ni muhimu ni wakati wa kutumia kila kona:FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa limesema udhibiti wa uvuvi ni hatua inayofanya kazi na inapasw kutumika kwa kiasi kikubwa kote duniani.

FAO imeyasema hayo katika ripoti yake iliyoitoa leo ambayo inahusu hali ya uvuvi duniani, ufugaji wa samaki , ukuaji wa uzalishaaji na matumizi na pia ikiaihi hatua za kuchukuliwa kuhakikisha uvuvi endelevu.

Shirika hilo linasema kote duniani matumizi ya samaki yamefikia kiwango cha juu kabisa ambapo kila mtu anatumia kilo 20.5 kwa mwaka kiwango ambacho kinatarajiwa kuongezeka katika miongo ijayo na kuonyesha jukumu kubwa la sekta hiyo katika uhakika wa chakula na lishe duniani.

Mwanamke akibeba samaki kutoka pwani huko Maharashtra, India.
UNDP/Dhiraj Singh
Mwanamke akibeba samaki kutoka pwani huko Maharashtra, India.

 

Ripoti hiyo imesisitiza kwamba ufugaji endelevu wa samaki na kuhakikisha mipango bora ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha mwenendo wa sasa hauongezeki.

Ifikapo mwaka 2030 ripoti inasema uzalishaji wa samaki unatarajiwa kuongezeka na kufikia tani milioni 204 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ukilinganisha na mwaka 2018 huku ufugaji wa samaki nao ukiongezeka kwa asilimia 46 duniani.

Akisistiza umuhimu wa sekta ya uvuvi mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu amesema “Samaki na bidhaa za uvuvi vinatambulika sio tu lishe bora duniani lakini pia kama bidhaa zisizochafua mazingira kwa kiasi kikubwa” akiongeza kuwa ni lazima ziwe kitovu za mikakati ya uhakika wa chakula na lishe duniani katika ngazi zote.

Kutokana na mlipuko wa janga la corona au COVID-19 ripoti inasema shughuli za uvuvi zinaweza kuwa zimeshuka kwa karibu asilimia 6.5, hasa kutokana na vikwazo na uhaba wa nguvu kazi kwa sababu ya dharura ya kiafya ya janga hili.

Ripoto imesisitiza hatua maalum zichukuliewe iki kuwepo na uvuvi endelevu ambao utahakikisha uhakika wa chakula na lishe duniani huku pia ukilinda mazingira na bayoanuwai ya bahari.