Tukiaadhimisha siku ya wafanyakazi duniani tuwakumbe wanaobeba mzigo wa COVID-19:Guterres

1 Mei 2020

 Katika sehemu mbalimbali duniani leo ni sikukuu ya wafanyakazi, na mwaka huu kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku hiyo imeghubikwa na janga la virusi vya corona au COVID-19, na kwa hakika imedhihirisha kwamba kuna wafanyakazi ambao mara nyingi hubeba mzigo mkubwa bila kuonekana.

 Amesema “Labda kuliko wakati mwingine wowote tunatambua jukumumuhimu linalofanywa na wafanyakazi katika kuhakikisha jamii zetu zinaendelea na Maisha, kuhakikisha kuna mlo mezani na masokoni, kuhakikisha usafiri wa umma unaendelea kufanyakazi na bila shaka kuhakikisha operesheni katika hospitali na mifumo ya afya zinaendelea.”

Guterres ameongeza kuwa siku hii pia inatukumbusha gharama kubwa iliyosababishwa na janga la COVID-19 katika sekta ya akazi duniani. Kama ilivyosema ripoti ya shirika la kazi duniani ILO wiki hii”Sekta ya ajira duniani itaathirika vibaya huku ajira milioni 300 zikipotea kutokana na janga hilo”.

Katibu mkuu amesisitiza kuwa wakati tukijitahidi kujikwamua kutokana na janga hili la corona, ustawi wa watu lazima uwe kitovu cha sera za uchumi na jamii huku kipaumbele kikitolewa kwa wale ambao wameachwa nyuma zaidi.

“Tunaweza kujenga utandawazi sawia ambao misingi yake ni usawa, uendelevu na haki. New mwelekeo ni kuenzi hadhi za ajira na sio kwa maneno tu bali kwa vitendo, na sio mara moja kwa mwaka lakini kila siku.”

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter