Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 imeathiri wafanyakazi katika kila nyanja:ILO

Wafanyakazi wachanga kiwandani wakitengeneza Shati nchini Ghana.
World Bank/Dominic Chavez
Wafanyakazi wachanga kiwandani wakitengeneza Shati nchini Ghana.

COVID-19 imeathiri wafanyakazi katika kila nyanja:ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO kuhusu athari za virusi vya corona au COVID-19 katika soko la ajira zinaonyesha kuna athari kubwa na mbaya kwa wafanyakazi wa sekta zisizorasmi za kiuchumi na kwa mamilioni ya makampuni duniani.

Takwimu mpya zilizotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO kuhusu athari za virusi vya corona au COVID-19 katika soko la ajira zinaonyesha kuna athari kubwa na mbaya kwa wafanyakazi wa sekta zisizorasmi za kiuchumi na kwa mamilioni ya makampuni duniani.

Takwimu hizo zinasema kuendelea kupungua kwa saa za kazi duniani kote kutokana na COVID-19 inamaanisha kwamba wafanyakazi bilioni 1.6 katika sekta isiyo rasmi ya kiuchumi ambayo ni karibu nusu ya wafanyakazi wa dunia wako katika hatari ya maisha yao kusambatratika.

Kwa mujibu wa takimu hizo katika ripoti ILO Monitor third edition: COVID-19 and the world of work , kupungua kwa saa za kazi katika robo hii ya pili yam waka 2020 kunatarajiwa kuwa kubaya Zaidi ya ilivyokadiriwa hapo awali.

Ikilinganishwa na robo ya nne yam waka 2019 kabla ya kuzuka kwa janga la corona hivi sasa inatarajiwa kushuka kwa asilimia 10.5 sawa na ajira milioni 3.5 zakutwa nzima ambazo watu hufanyakazi ya saa 48 kwa wiki.

ILO inasema hapo awali makadirio yalikuwa ajira kushuka kwa asilimia 6.7 sawa na wafanyakazi wa kutwa nzima milioni 195 na hii ni kutokana na kuongezwa kwa muda wa watu kujitenga na kusalia majumbani.

Hali ni mbaya kila kanda

ILO inasema hali imezidi kuwa mbaya katika kanda zote na makadirio yanaonyesha kwamba kutakuwa na asilimia 12.4 ya kupoteza saa za kazi katika robo ya pili yam waka huu kanda ya Marekani ikilinganishwa na kabla ya kuzuka kwa janga hili na kwa Ulaya na Asia ya kati kutakuwa na punguzo la asilimia 11.8 ya saa za kazi na kwingineko ni zaidi ya asilimia 9.5

Wanawake wafanyakazi katika kampuni ya dawa huko Moldova
World Bank/Victor Neagu
Wanawake wafanyakazi katika kampuni ya dawa huko Moldova

 

Athari za uchumi usio rasmi

Kutokana na janga la COVID-19 jumla ya wafanyakazi bilioni 1.6 kutoka uchumi usio rasmi kati ya jumla ya ajira bilioni mbili na wafanyakazi bilioni 3.3 duniani kote wameathirika katia kiwango cha kupata mapato ya kuwawezesha kuishi.

Hii imetokana na hatua za kuzuia kusambaa kwa maambukizi au ni kwa sababu wanafanyakazi katika sekta ambazo zimeathirika Zaidi na janga hili.

Mwezi wa kwanza wa njanga hili ILO inakadiria kuwa kulikuwa na kushuka kwa asilimia 60 kwa kipato katika wafanyakazi wasio rasmi duniani kote nah ii ni saw ana kushuka kwa asilimia 81 Afrika na Marekani, asilimia 21.6 Asia na Pasifiki na asilimia 70 Ulaya na Asia ya Kati.