Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 si ukomo wa masomo kwa wakimbizi

Kambini Dadaab
UNHCR
Kambini Dadaab

COVID-19 si ukomo wa masomo kwa wakimbizi

Utamaduni na Elimu

Nchini Kenya matangazo ya shule kwa njia ya redio sasa yameanza katika kambi za wakimbizi ambapo walimu wanafundisha masomo kupitia redio za jamii ili wanafunzi waendelee na masomo hata wakati huu wa kusalia nyumbani kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.

Kambini Dadaab nchini Kenya, mwalimu Amina Hassan akiwa katika studio ya Radio Jamii ya Gargaar, tayari kufundisha wanafunzi wake wa darasa la 5 wapatao 100 somo la kiingereza.

Mafunzo haya ni mbinu iliyoibuliwa na serikali ya Kenya kwa kushirikiana na wadau kama vile shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNCR wakati huu ambapo virusi vya Corona vimesababisha kufungwa kwa shule kwa muda usiojulikana, lakini masomo lazima yaendelee.

Mwalimu Amina badala ya kufundishia darasani kama alivyozoea, sasa amelazimika kuingia studio kufundisha wanafunzi ambapo anasema,

“Si wote wenye redio lakini wakati ukifika wanaweza kupata redio ya kuweza kufuatilia.”

Mafunzo kwa njia ya redio ambapo wanafunzi wanakaa vikundi vikundi kufuatilia wakiwa na kalamu na madaftari, yanasaidia walimu kambini Daadab kufikia wanafunzi zaidi ya 100,000 ambao ni wanafunzi katika shule 22 za msingi na 9 za sekondari kambini Dadaab.

Amina anasema kuwa,

“Kutokana na virusi vya Corona, shule zimefungwa lakini elimu lazima iendelee badala ya kukoma.”