Nilikuwa nakufa, wahudumu wameniokoa-aliyepona COVID-19

28 Aprili 2020

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mmoja wa manusura wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 amesihi raia wa taifa hilo la Maziwa Makuu Afrika waitikie wito wa kujikinga na gonjwa hilo akisema kuwa yeye ni shuhuda aliyenusurika.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mmoja wa manusura wa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 amesihi raia wa taifa hilo la Maziwa Makuu Afrika waitikie wito wa kujikinga na gonjwa hilo akisema kuwa yeye ni shuhuda aliyenusurika.

Manusura huyo Adrien Bali mwenye umri wa miaka 56 amesema haoy akizungumza kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kwenye mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Bwana Bali ambaye alipata huduma kwenye hospitali ya Mtakatifu Joseph jijini Kinshasa anasema kuwa, “nilikuwa mwenye afya njema lakini asubuhi ya jumapili kabla ya Pasaka, wakati nataka kunywa chai, nilikosa kabisa hamu ya kuinywa. Niliona chakula kama tope na sikuweza kumeza kitu chochote. Siku ya jumatatu, nilianza kukosa pumzi na jioni ilipofika sikuweza kupumua kabisa.”

Bali ambaye anatoka wilaya ya Limete jijini Kinshasa ameendeleza simulizi yake akisema kuwa, Jumanne nilikuwa nakufa, nilishindwa kupumua. Nilimpigia simu daktarin wangu ambaye ilibidi azungumze na mke wangu kwa sababu sikuweza kuendelea kuzungumza naye. Lakini nilinikuwa nakufa. Ilikuwa ni virusi vya Corona, sikuweza kupumua. Kama wasingaliniwekea mashine ya kunisaidia kupumua nilikuwa nakufa. Kwa hiyo huduma katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ni nzuri sana.”

Kupona kwa Bwana Bali, kumempatia fursa ya kupaza sauti kwa raia wa DRC akiwaambia kuwa, Natoa wito kwa wakongo wenzangu, kwa sababu ni manusura, tafadhali tambuein umuhimu wa kuvaa barakoa na kutochangamana, muwe umbali unaotakiwa ili tuondokane na janga hili.”

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, DRC ina jumla ya wagonjwa 459 ambapo kati yao hao  28 wamefariki dunia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter