Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana ni chachu ya mabadiliko na raia wenye haki sawa na wengine:Guterres

Vijana wamuuliza maswali Katibu Mkuu Antonio Guterres wakati wa mkutano wa UN75 huko Geneva
UN Photo - Jean-Marc Ferre
Vijana wamuuliza maswali Katibu Mkuu Antonio Guterres wakati wa mkutano wa UN75 huko Geneva

Vijana ni chachu ya mabadiliko na raia wenye haki sawa na wengine:Guterres

Amani na Usalama

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antoni Guterres amesema vijana wanapaswa kuwa raia wenye haki sawa na raia wengine, wajumbe kamilifu wa jamii na mabalozi wenye nguvu ya kuleta mabadiliko.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antoni Guterres amesema vijana wanapaswa kuwa raia wenye haki sawa na raia wengine, wajumbe kamilifu wa jamii na mabalozi wenye nguvu ya kuleta mabadiliko.

Guterres ameyasema hayo katika ripoti yake ya kwanza kwenye kikao maalum cha Baraza la Usalama la Umoja wa Msataifa kuhusu vijana amani na usalama .

Ameongeza kuwa tangu kutolewa kwa ripoti hiyo dunia imetikiswa na janga la virusi vya Corona au COVID-19. Na kwamba vujana wanahisi athari zake kwa kiasi kikubwa kuanzia kupoteza ajira, msongo wa mawazo ya kifamialia hadi afya ya akili na changamoto zingine.

Amerejerea kusema kwamba “Dunia haiwezi kumudu kuwa na kizazi kilichopotea cha vijana, Maisha yao kurejeshwa nyuma na janga la COVID-19 na sauti zao kuzima napengo la kutoshirikishwa”

Hata hivyo Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la Usalama kwamba wakati huu mgumu vijana bado wanasaka mbinu za kushiriki, kusaidiana na kudai na kuleta mabadiliko. Amepongeza majukumu yao katika vita dhidi ya COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi.

UN inafanya kila njia kushirikisha vijana

Licha ya yote Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa unafanya kila liwezekanalo kujumuisha ajenda ya vijana , amani na usalama katika shirika zima, ukiongozwa na mkkati maalum wa vijana wa Umoja wa Mataifa ingawa bado unakabiliwa na changamoto. “Fursa za ushiriki bado hazitoshi. Vijana wengi wajenzi wa amani wanaripoti kwamba ushiriki wao haukaribishwi na umma au wale walio madarakani. Hili ni Dhahiri shairi hasa kwa wasichana. Kutengwa katika maamuzi ya kisiasa kunaongeza fursa ya ubaguzi, ukatili wa kijinsia na manyanyaso, usafirishaji haramu wa binadamu na ndoa za utotoni.”

Guterres ameendelea kusema kwamba “assilimia 2.2 pekee ya wabunge duniani ndio walio chini ya umri wa miaka 30. Hivyo haishangazi kushuhudia kupungua kwa idadi ya wapiga kura vijana kwenye vyama kote duniani, ikidhihirisha kutoridhishwa  na mwenendo wa kisiasa.”

Mwakilishi wa vijana wa UN

 Aliyezungumza kwenye kikao hicho pia ni mwakilishi maalum wa vijana wa Umoja wa Mataifa Jayathma Wicramanayake ambaye taarifa yake imejikita Zaidi kwa vijana wote ambao wanaziweka jamii zao mbele badala ya maslahi yao binafsi katika maeneo ya mizozo, kwenye makambi ya wakimbizi, kwenye misukosuko na kwenye makazi ambako wanaonyesha uongozi ambao wakati mwingine dunia inashindwa kuuona kwa viongozi wa kisiasa.

Mwaka huu ni miaka mitano tangu kupitishwa kwa azimio 2250 linalohusu vijana amani na usalama mwakilishi huyo amesema hii ni fursa nzuri ya kutathimini kuhusu ajenda hiyo.

Wicramanayake amezungumzia pia mapendekezo ambazo yanaunga mkono sauti za vijana aliokutana nao na kusistiza kwamba “ushiriki wenye maana kwa vijana katika kujenga amani endelevu ni lazima uhakikishwe. Ushiriki unatambulika kama haki ya binadamu . Vijana wote wana haki ya kushiriki katika masuala ya mwenendo wa umma na kwamba wana haki ya kuwa na uhuru.”

Akaenda mbali zaidi na kusema ushiriki huo unajumuisha “kuchukuliwa kwa hatua mbalimbali kuanzia ushiriki rasmi katika siasa, mchakato wa uchaguzi hadi kwenye ushiriki usio rasmi katika ngazi ya jamii na majukwaa ya kidijitali. Maeneo ya kuwawezesha vijana lazima yaandaliwe ambako wanaonekana na kuheshimika kama raia wenye haki sawa, sauti saw ana ushawishi sawa.”

Mwakilishi huyo ameongeza kuwa vijana wanaamini kwamba mfumo maalum na imara unahitajika ili kuwalinda vijana wanaharakati na wajenzi wa amani, na hivyo ametoa wito kwa nchi wanachama kusaidia kuwezesha na kujumuisha, usalama, uwezeshaji na mazingiza yanayoheshimu usawa wa kijinsia ambayo vijana wajenzi wa amani na watetezi wa haki za binadamu wanatambuliwa na wanapewa msaada na ulinzi kuweza kufanya kazi zao kwa uhuru bila kuingiliwa.

Wicramanayake amehitimisha kwa kusema kwamba “Hatuwezi kumudu kupoteza Imani ya vijana, ambao ni lulu na matumaini ya mustakabali bora wa dunia hii.”.

Na kwa upande wa Baraza la Usalama amelitaka kuwaweka vijana katika kitovu cha juhudi zake za kuleta amani na usalama duniani.