Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yatoa ombi kupiga jeki masuala ya kiufundi ambayo ni muhimuli wa vita dhidi ya COVID-19 

Wahudumu wa afya wapokea vifaa tiba kutoka kwa UNICEF huko Jakarta kwa ajili ya kukabiliana na COVI-19
© UNICEF/Arimacs Wilander
Wahudumu wa afya wapokea vifaa tiba kutoka kwa UNICEF huko Jakarta kwa ajili ya kukabiliana na COVI-19

UN yatoa ombi kupiga jeki masuala ya kiufundi ambayo ni muhimuli wa vita dhidi ya COVID-19 

Afya

Wakuu wa mashirika makubwa ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadammu na ofisi mbalimbali leo wamezindua ombo la dharura kwa ajili ya kukusanya dola milioni 350 kusaidia vituo vya kimataifa vya misaada kwa ajili ya watu walio katika hatari zaidi wakati huu wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Kupitia barua ya wazi iliyochapishwa Jumapili na gazeti la Uingereza la The Guardian, wakuu hao wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo shirika la afya duniani WHO, na la mpango wa chkula duniani WFP, Pamoja na ofisi ya kutratibu masuala ya kibinadamu na dharura OCHA wamesema kufutwa kwa safari za ndege na safari za kusafirisha misaada kumechagiza ombili hulo ili kuwezesha kuongeza kasi ya kwafanyakazi na usambazaji wa misaada katika maeneo ambayo yameathirika vibaya na virusi vya corona.

Mashirika hayo yanasema nchi zinazoendelea ambazo zina uwezo mdogo wa kudhibiti virusi vya Corona inaweza kuwa ni upenyo kwa ugonjwa huo na huenda ikazusha wimbi jipya za mlipuko wa COVID-19 kote duniani, wameonya wakuu hao wa mashitika wakisema kwamba “bila nyezo hizi hatua za kimataifa kupambana na janga hilo zinaweza kupata pigo.”

Mkuu wa OCHA Mark Lowcock amesema mashirika ya misaada ya kibinadamu hufanyaazi katika maeneo ambako kuna changamoto kubwa ambako kudhibiti virusi hivyo ni vigumu. “Hakuna mtu atakayekuwa salama hadi pale kila mtu atakapokuwa salama.” Ameongeza kuwa hii sio tu kwa sababu ya huruma au utu ni kwa sababu ya dhamira binafsi.”

Kwa upande wake shirika la WFP limesema linahitaji kupanua wigo wa usafirishaji wake na huduma za kiufundi ikiwemo huduma za kibinadamu za usafiri wa anga ambazo zinapatikana kwa wahudumu wote wa kibinadamu.

Lengo shirika hilo linasema ni kutumia vituo viwili vya usafiri wa biashara barani Ulaya ili kupata ndege za kusafirisha wahudumu wa kibinadamu katika maeneo yenye migogoro ikiwemo Mashariki ya Kati na Afrika.

Pia inalenga kusafirisha watu kwenda kwenye hospitali saba duniani ambayo ziko mashinani zinazohudumia wahudumu wa misaada ya kibinadamu ambao wataathirika na virusi vya Corona wakiwa kazini.


Ombi la msaada

Ombi hili la msaada limekuja baada ya miezi ya nchi kusaka mbnu zao wenyewe baada ya taasisi nyingi za kimataifa za kisiasa ikiwemo za Muungano wa Ulaya zikijikokota kufikia muafaka.

Pia barua hiyo imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuzindua omb la dola bilioni 2 mnamo Machi 25 ambalo hadi sasa n idola milioni 550 tu ndizo zilizoahidiwa , katikati ya hatua ya Rais Donald trump wa Marekani kusitisha ufadhili kwa WHO shirika la Umoja wa Mataifa linaloongoza vita dhidi ya virusi vya Corona.

Tofauti katika athari

Barua hiyo imetoa taswira ya virusi vya corona kama moja ya changamoto kubwa unayoukabili ubinadamu tangu vita vya pili vya dunia, ikitaja kwamba havitambui mipaka, kuiacha nchi yoyote ay bara na havibagui.
“Katika mbio hizi dhidi ya adui aiyeonekana nchi zote lazima zipambane lkini sio zote zinazoanzia kwenye msitari mmoja.imesema kwamba katika nchi ambazo watu wengi hawajiwezi wanahitaji msaada kudhibiti janga hili , na kufutwa kwa safari za ang ana usambazaji wa misaada kumewaathiri zaidi.”
Barua hiyo imesisitiza kwamba ni kwa faida ya kila mmoja kukomesha kusambaa kwa virusi hivi ambavyo vinasambaratisha Maisha na uchumi na kuendelea kuzunguka duniani kote.
Barua imeongeza kuwa huduma inayotolewa na WFP kwa niaba ya jumuiya ya misaada ya kimataifa itawezesha mchakato unaotosheleza kupambana na COVID-19 kwa watu wasiojiweza kabisa.