Kenya yaendelea kuchukua hatua huku idadi ya wagonjwa wa Corona ikifikia 281

20 Aprili 2020

Huku vita dhidi ya ugonjwa wa  corona au COVID-19 vikipamba moto kote duniani, nchini Kenya hatua za kukabiliana na ugonjwa zinaendelea wakati huu ambapo  idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo imeongezeka na kufika watu 281. Hii ni baada ya wagonjwa wengine 11 kuthibitishwa hii leo.

  Huku vita dhidi ya viuusi vya corona vikipamba moto kote duniani, huko Kenya sasa idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo imefika watu 281. Hii ni baada ya wagonjwa wengine 11 kuthibitishwa hii leo. Hata hivyo wizara ya afya nchini humo imetangaza kuwa itawafanyia watu zaidi uchunguzi kila siku kubaini ni maeneo yapi yaliyoathirika kwa kiwango kikubwa. Jason Nyakundi anayo taarifa zaidi

Wizara ya afya nchini Kenya imetangaza kuwa vituo vya kuwafanyia watu uchuguzi dhidi ya virus vya korona vitaongezwa ambapo kila kaunti itakuwa na takriban mahabara moja.

Akiongea na waandishi wa habari waziri wa afya mutahi kagwe alisema vituo 33 vya karantini kote nchini Kenya kwa sasa vinawazuia jumla ya watu 483.

UNEP/Nicholas Greenfield
Siddharth Chatterjee, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya na wawakilishi kutoka serikalini katika hafla ya ombi la fedha kwa ajili ya kukabiliana na COVID-19.

Bw Kagwe amesema watu wengine 455 wamewekwa katika karantini ya lazima baada ya kukiuka amri ya serikali ya kuwataka kubaki manyumbani mwao hasa usiku.

Waziri amewaonya wale wanaokiuka amri za serikali wakati zinapoendelea jitihada za kupambana na virusi hatari vya corona.

 

Wakati huo huo idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya corona hadi sasa imeongezkea hadi watu 281 kufuatia kuthibitishwa  wagonjwa 11 zaidi.

Kati ya hao 11,  5 ni wanawke na 6 wanaume wote walio kati ya umri wa miaka 11 na 80.

Waziri Kagwe amesema saba kati ya wagonjwa wako Mombasa huku wanne wakiwa Nairobi.

Kagwe pia ametangaza kuwa wagonjwa 2 zaidi, kati yao akiwa ni daktari wamepona na kufikisha idadi ya wagonjwa waliopona virusi vya korona nchini Kenya kuwa watu 69

Hadi sasa jumla ya watu 14 wamefaraki kutokana na virusi vya Corona nchini Kenya.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud