Chuki na unyanyapaa vimeongezeka wakati huu wa COVID-19:Achiume

16 Aprili 2020

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya masuala ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni , ubaguzi na hali zingine za kutovumiliana  profesa Tendayi Achiume amesema wakati huu wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 hali hizi zimedhihirika kuongezeka.

Akizungumza na UN News Bi.Achiume amesema makundi yanayolengwa na ubaguzi na chuki hizo ni yale ambayo kwa muda mrefu yamekuwa waathirika wa vitendo hivyo vya kibaguzi,“Katika hali ya dharura kama hii mara nyingi matatizo ambayo yalikuwepo yanaongezeka , makundi memgi ni yale ambayo tayati yalikuwa yanakabiliwa na ubaguzi, chuki na hali ya kutovumiliana chukulia mfano Waasia wenye asili Marekani hivi sasa , Waafrika ambao wanakabiliwa na hatua mbalimbali China hivi sasa kwa ajili ya kukabiliana na COVID-19, wafikirie Waroma ambao wanalengwa katika nchi mbalimbali za Ulaya wakishutumiwa kusambaza virusi na kukabiliwa na hatua kali.”

Amesema hata katika masuala muhimu kama upimaji kwa mfano kuchagua nani  apimwe badala ya kuzingatia sayansi na hali halisi inaruhusuubagui huo kupanua wigo n ahata kuingia kwenye sera haki ambayo inaiweka jamii nzima kwenye changamoto na hilo ni tatizo kubwa. Na je changamoto ni ipi katika kukabiliana na ubaguazi na unyanyapaa huu hasa wakati huu wa COVID-19 Bi. Achiume anasem, “Sehemu ya changamoto ni kuwafanya watu kuwaona watu wengine kama binadamu na pia kuoanisha jinsi wewe unavyokabiliwa na ubaguzi na wengine wanavyokabiliwa na ubaguzi”

Ameongeza kuwa Pamoja na serikali, viongozi wa kijamii na sekta mbalimbali vyombo vya Habari pia vina wajibu mkubwa katika kupambana na ubaguzi na chuki kuanzia kwenye vyombo vya Habari vya kawaida hadi kwenye mitandao ya kijamii.  Nini kifanyike sasa kuhakikisha jamii nayo inatambua na kuachana na ubaguzi?“Nadhani elimu ndio suluhu hapa , kuwaona watu wengine kama watu , makundi mengine kama binadamu , ndio itakuwa vigumu kujihusisha na vitendo hata vidogo vya ubaguzi. Napenda kuamini hivyo na kama sivyo basi tuko kwenye tatizo kubwa.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter