Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN iko pamoja na nchi za Pacific zilizopigwa na kimbunga Harold-Guterres

Wakati kimbunga kilipokaribia kupiga eneo la Suva, Fiji
UNICEF/UN010591/Clements
Wakati kimbunga kilipokaribia kupiga eneo la Suva, Fiji

UN iko pamoja na nchi za Pacific zilizopigwa na kimbunga Harold-Guterres

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo jumapili kupitia msemaji wake, ametuma salamu zake za rambirambi pamoja na kusikitishwa kwake kutokana na kimbunga Harold ambacho kimezipiga nchi za visiwa vya Pacific na kusababisha upotevu wa maisha na mali.

Msemaji wa Bwana Guterres amesema kuwa wakati dunia inapambana kushughulika na madhara mabaya ya virusi vya corona, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasikitishwa sana na ripoti za kupotea kwa maisha pamoja na uharibifu mwingine uliosababishwa na kimbunga Harold.

Kwa mujibu wa ripoti, kimbunga cha kitropiki kilichopewa jina Harold kilipiga nchi za visiwa vya Pacific siku nne zilizopita na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na miundombinu ya Vanuatu, Fiji, visiwa vya Solomon na Tonga na kuwaathiri watu wengi. Hivi sasa watu hao wana uhitaji wa haraka wa makazi, maji, vifaa vya kujisafi na chakula, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Bwana Guterres ameipongeza serikali pamoja na wafanyakazi wa dharura wan chi ambazo zimeathirika kwa uharaka na namna walivyoshughulika kuhakikisha usalama wa watu na kufikiwa kukidhi mahitaji ya watu kabla ya dhoruba. 

“Umoja wa Mataifa umejitaziti kuunga mkono juhudi hizi.” Taarifa imemnukuu Bswana Guterres.

Katibu Mkuu Guterres kupitia taarifa hiyo ameeleza mshikamano wake na watu wa nchi za visiwa vya Pacific ambao wamekumbwa na madhara ya kimbunga pamoja na changamoto nyingine zinazohusiana na tabianchi pamoja na  kuongezeka ugonjwa wa COVID-19 ambao unaongeza wasiwasi.