Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wajibu wetu kuwalinda wakimbizi dhidi ya COVID-19-UNHCR

Kambini Kakuma
UN/Esperanza Tabisha
Kambini Kakuma

Ni wajibu wetu kuwalinda wakimbizi dhidi ya COVID-19-UNHCR

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linachukua tahadhari zote na kufanya kila liwezalo ili kuwalinda wakimbizi walio katika makambi mbalimbali ya wakimbizi barani Afrika dhidi ya janga la virusi vya Corona, COVID-19.

Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini wakimbizi wakipangwa katika mistari maalum umbali wa mita moja wakisubiri kupata mgao wa chakula huku wakipatiwa maelekezo maalum ya kujikinga na virusi vya Corona, COVID-19 na pia kupimwa joto la mwili.

Natts……….

Shirika hilo la wakimbizi linasema ingawa idadi ya wagonjwa walioripotiwa kuwa na virusi hivyo na kuthibitishwa barani Afrika ni ndogo, lakini zaidi ya asilimia 80 ya wakimbizi na karibu wakimbizi wote wa ndani wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha wastani nchi ambazo nyingi mifumo yake ya afya, maji, na mifumo ya usafi ni duni na wanahitaji msaada wa haraka.

Mbali ya kambi ya Kakuma Kenya kambi zingine ambako hatua madhubuti zinachukuliwa hivi sasa ni kambi ya Mtabila nchini Tanzania, kambi ya Nampula nchi Msumbiji, kambi ya wakimbizi wa ndani ya Juba Sudan kusini na kambi ya wakimbizi ya West Darfur nchini Sudan.

Natts….

Kwenye kambi ya Mtabila Kigoma Tanzania miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na UNHCR ni kuwanapatia wakimbizi elimu ya kunawa mikono kwa sababuni na kuzingatia usafi. Pia wanagawa sabauni hizo na kuongeza fursa ya upatikanaji wa maji.

Kwa nchi za Msumbiji, Sudan Kusini na Sudan pamoja na hatua kama hizi pia kutoa mafunzo kwa waelimishaji wa kijamii ambao watawafunza wakimbizi jinsi ya kujilinda na virusi hivyo.

Pamoja na kuchukua hatua zote hizo UNHCR iinazisaidia serikali katika hatua za kuzuia na huduma za afya za kukabiliana na COVID-19 ikiwa ni pamoja na kuwapa vifaa vya kitatibu na kuhakikisha taarifa muhimu kuhusu mlipuko huu zinapatikana na kuwafikia wakimbizi kwa urahisi.

Shirika hilo linasema linaendelea pia kutoa vifaa vya malazi na vifaa vingine muhimu pamoja na kuhakikisha kwamba haki za wakimbizi , wakimbizi wa ndani na watu waliolazimika kukimbia makwao zinaheshimiwa na kulindwa.