Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria: pande kinzani zimeshindwa kutimiza sheria za kimataifa kuhusu kushambulia hospitali 

Picha ya maktaba ikionesha kiliniki za kuhamahama zilizotolewa na WHO ili kusambaza huduma ya afya kwa watu wanaokimbia vurugu mjini Aleppo Syria
WHO Syria
Picha ya maktaba ikionesha kiliniki za kuhamahama zilizotolewa na WHO ili kusambaza huduma ya afya kwa watu wanaokimbia vurugu mjini Aleppo Syria

Syria: pande kinzani zimeshindwa kutimiza sheria za kimataifa kuhusu kushambulia hospitali 

Amani na Usalama

Pande kinzani katika vita vya Syria ambavyo vimeingia mwaka wa kumi sasa zimeshindwa kutimiza wajibu wao chini ya sharia za kimataifa wa kuepuka kushambulia hospitali na vituo vingine vya raia ambavyo vimeorodheshwa katika orodha ya Umoja wa Mataifa amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Guterres ameyasema hayo katika muhitasari wa ripoti ya kurasa 185 kutoka bodi ya uchunguzi kuhusu vita vya Syria iliyoanzishwa Agosti Mosi mwaka jana ikielezea matukio kadhaa yaliyotokea Kaskazini Magharibi mwa Syria yakihusisha vituo katika orodha ya maeneo yasiyostahili kushambuliwa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na vituo vinavyosaidiwa na Umoja wa Mataifa.


Maeneo yaliyo katika orodha yanapaswa kutolengwa na operesheni za kijeshi kwa sababu yanahusisha vituo vya afya au shughuli zingine za raia au vinasaidiwa na Umoja wa Mataifa.


Katika barua kwa Jose singer Weisinger wa Jamhuri ya Dominika ambaye ni Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Aprili,  Bwana Guterres amesema “Athari za vita hivyo kwa rai ana maeneo ya kibinadamu Kaskazini Magharibi mwa Syria ni kumbusho la wazi la umuhimu kwa pande zote katika mzozo kuzingata na kuhakikisha zinaheshimu sharia za kimataifa za binadamu.”


Tofautisheni baina ya rai na wapiganaji


Hilo linajumuisha wajibu wa kila wakati wa kutofautisha baina ya rai ana wapiganaji na baina ya vitu vya rai ana wanajeshi na mashambulizi ya moja kwa moja ni kwa wapiganaji tu na vitu vya kijeshi amesema Katibu Mkuu.
“Kwa mujibu wa ripoti kadhaa pande kinzani zimeshindwa kutimiza haya” akisisitiza kwamba hatua zozote zinazochukuliwa nan chi wanachama kukabiliana na ugaidi zinapaswa kwenda sanjari na wajibu wao chini ya sharia za kibinadamu za kimataifa , haki za binadamu na sharia za wakimbizi.


Bodi hiyo ya uchunguzi ya wajumbe watatu inayoongozwa na Luten Jenerali msataafu wa Nigeria Chikabidia Obiakor ilitokana na matukio kadhaa yaliyotripotiwa Kaskazini Magharibi mwa Syria tangu Septemba 2018 ambapo Urusi na Uturuki walitia Saini maelewano ya kurejesha utulivu katika eneo la Idlib ambako ni maskani ya mwisho ya waasi waliosalia.


Ripoti hiyo na mapendekezo yake inampa Katibu Mkuu msingi wa kufikiria nini atafanya ili kuwalinda vyema rai ana kudhibi rasilimali za shirika katika eneo hilo.


Ripoti piaimeeleza kwamba ilikuwa vigumu kuzuru hata eneo moja timu hiyo ilikotakiwa kuzuru baada ya serikali ya Syria kushindwa kujibu maombi yao ya kufanya hivyo.


Lakini kutokana na taarifa kutoka kwa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa , mashirika yasiyo ya kiserikali, mashahidi na vyanzo vingine tume hiyo imeweza kukusanya taarifa za matukio yaliyitokea katika maeneo sita.


Vituo vitano huenda vilishambuliwa na serikali na washirika wake 


Kutokana na taarifa zilizopatikana bodi hiyo ya uchunguzi imesema kwamba inawezekana kwamba shambulio katika kituo cha huduma za afya za msingi cha Rakaya kwenye Kijiji cha Rakaya Sijneh jimbo la Idlib mnamo 3 Mei 2019 lilifanywa na vikosi vya serikali.


Imeongeza kuwa inawezekana pia kwamba uharibifu kwenye kituo kama hicho kwenye eneo la Kafr Nabutha jimbo la Hama hapo 7 Mei 2019 liliendeshwa na vikosi vya serikali na washirika wake.


Katika shambulio kwenye kambi ya wakimbizi ya Wapalestina ya Nayab karibu na Aleppo 14 Mei 2019 amnapo watu 11 waliuawa na wengine 29 kujeruhiwa bodi hiyo inasema inawezekana shambulio hilo la anga lilifanywa na ama vikosi vyenye silaha vya upinzani au Hayat Tahrir al-Sham kikundi chenye itikadi kaliambacho kimetajwa kama kikundi cha kigaidi na Baraza la Uslama.


Kuhusu uharibifu kwenye kituo cha kitabibu cha upasuaji kwenye Hospitali ya Kafr Nobol jimbo la Idlin 4 Julai mwaka jana tume hiyo ya uchunguzi imesema kuna uwezekano mkubwa shambulio hilo la anga lilifanywa na vikosi vya serikali au washirika wake. Lakini imesema imekosa Ushahidi wa kutosha kuhitimisha kwa hakika.
Bodi hiyo imesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba shambulio dhidi ya kituo cha ulinzi wa Watoto cha Ariha jimbo la Idlib lililofanyika 28 Julai 2019 lilifanywa na vikosi vya serikali na au washirika wake ingawa haina Ushahidi wa kutosha kuhitimisha hilo.


Tume hiyo haikuangalia tukio la saba katika hospitali ya taifa ya as-Suqlabiyah, jimbo la Hama manamo 26 Mei 2019 kwa sababu haikuwa katika orodha ya Umoja wa Mataifa au kusaidiwa na Umoja wa Mataifa.