Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali ya taifa Tanzania, Muhimbili yatenga sehemu maalum kwa ajili ya kunawa mikono

Mradi wa sehemu ya kunawa mikono kwa ufadhili wa Mo Dewj Foundation nchini Tanzania.
UN News/ UNIC Dar es Salaam
Mradi wa sehemu ya kunawa mikono kwa ufadhili wa Mo Dewj Foundation nchini Tanzania.

Hospitali ya taifa Tanzania, Muhimbili yatenga sehemu maalum kwa ajili ya kunawa mikono

Afya

Tanzania kama ilivyo katika mataifa mengine imeweka mikakati kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19. Hatua mbali mbali zinachukuliwa na serikali na pia mashirika binafsi yanaunga mkono juhudi za serikali. Afisa wa maswasiliano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Saalam, UNIC ametembelea hospital ya taifa ya Muhimbili kushuhudia baadhi ya mikakati iliyowekwa kama sehemu ya juhudi za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo

Nipo hapa katika hospital ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo kama ilivyo ada shughuli za kila siku zinaendelea. Kila siku hospital hii hupata wageni wengi ambao wanakuja kutembelea wagonjwa huku wengine wakifika hapa kusaka matibabu. Lakini mlipuko wa virusi vya corona umebadilisha taswira ya hospital hii kama anavyoafiki Musa Hamisi

(Sauti ya Musa)

 

Uwepo wa sehemu hii ya kunawa mikono katika hospital ya Muhimbili ni kwa ufadhili wa Mo Dewj Foundationa Rachel Chengula ambaye ameelezea umuhimu wa wao kutengeneza sehemu ya kunawa mikono

(Sauti ya Rachel)