Skip to main content

Hakuna COVID-19 katika kambi ya Zaatar lakini tumeanza kujipanga-UNHCR

Mwonekano wa kambi ya wakimbizi wa Syria, Zaatari huko kaskazini mwa Jordan
UN News
Mwonekano wa kambi ya wakimbizi wa Syria, Zaatari huko kaskazini mwa Jordan

Hakuna COVID-19 katika kambi ya Zaatar lakini tumeanza kujipanga-UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

UNHCR imesema inafanya kazi na wizara ya afya ya Jordan kuandaa mazingira ya kupambana na virusi vya corona. 

Iyad Shyauiat, ambaye ni Afisa afya katika UNHCR anasema, “tunawapa mwongozo kuhusu taratibu wanazozifanya ndani ya kiliniki zao kwa maana ya kudhibiti maambukizi na kujiandaa na utayari.”

UNHCR imesema hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote wa COVID-19 ambaye ameshapatikana miongoni mwa wakimbizi ndani ya kambi lakini hospitali ndani ya kambi ambayo inawahudumia wakimbizi wa Syria takribani 76,000, inajiandaa kwa mlipuko wa ugonjwa huo.

Taha Abu ni daktarin katika hospitali kambini hapo anasema,“wagonjwa wengi wanaokuja katika chumba cha dharura wana magonjwa yanayohusiana na mafua. Dawa zipo, UNHCR haina upungufu. Hali ni nzuri tunamshukuru Mungu, watu wanafurahi.”

Iyad Shyauiat afisawa UNHCR anasema mategemeo ni kwa wakimbizi  utegemezi kufuata ujumbe wa UNHCR kwa jamii kuhusu kuzuia COVID-19 ili kuzuia kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo wa virusi vya corona katika kambi.