Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ilibaki miezi michache nihitimu Chuo Kikuu, nikaikimbia Nicaragua- Arturo Martinez

Picha ya mwaka 2018 ikiwaonesha waandamanaji mjini Managua Nicaragua, bango moja la sema, walikuwa wanafunzi sio wahalifu.
Artículo 66
Picha ya mwaka 2018 ikiwaonesha waandamanaji mjini Managua Nicaragua, bango moja la sema, walikuwa wanafunzi sio wahalifu.

Ilibaki miezi michache nihitimu Chuo Kikuu, nikaikimbia Nicaragua- Arturo Martinez

Wahamiaji na Wakimbizi

Arturo Martinez alikuwa amesaliwa na miezi michache kabla ya kuhitimu Chuo Kikuu wakati alipojiunga na maandamano ya kuipinga serikali dhidi ya serikali ya Nicaragua. Kutokana na kitendo hicho, alipigwa, kutishiwa na kulazimishwa kuyaacha masomo yake kisha kuikimbia nchi. Hivi sasa akiishi Costa Rica, anapambana kuyajenga upya maisha yake. 

Kwa sababu ya maandamano ya kupinga serikali ya zamani ambayo yalitokea Nikaragua mnamo Aprili 2018, waandamanaji na wakati mwingine familia zao na marafiki, walikandamizwa vikali na vikosi vya usalama na vikundi vya watu waliokuwa wakiinga mkono serikali. Walengwa walikuwa ni pamoja na wanafunzi, madaktari, walimu, wakulima, waandishi wa habari na wanachama wa asasi za kiraia. Katikati ya ukatili huo, mamia waliuawa na maelfu walijeruhiwa. Arturo Martinez alikuwa katika miezi yake ya mwisho ya masomo anasema,“Jamaa alianza kunipiga akilenga bunduki kwangu akisema, ‘nitakuua’. Waliniweka katika chumba chenye giza. Walinipiga na kunitisha. ‘Tutaiua familia yako, tutawaua wazazi wako.’ Nilishikiliwa kwa siku 18.”

Arturo alipata usalama nchini Costa Rica lakini amehangaika tangu alipoachana na masomo yake. Kwa kadri idadi ya wale wanaokimbia inavyoongezeka, Costa Rica kwa kusaidiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, inaendelea kuwahifadhi maelfu ya watu wa Nicaragua na kuwapatia usalama na ulinzi, hivyo kuwasogeza wanafunzi kama Arturo angalau hatua moja karibu na kuyajenga upya maisha yao. Arturo anaeleza,“Ilikuwa vigumu sana kwasababu sikuwa na yeyote Costa Rica. Nikiwa nimepoteza kila kitu nilichokifanyia kazi, nilijihisi kama sikuwa na chochote. Nilikaribia kujiua.”

Hata hivyo kijana huyo bado ana matumaini,“Sijui kile ambacho maisha ya siku za usoni yanacho kwa ajili yangu. Ninachoweza kufanya ni kusonga mbele.”

Zaidi ya raia wa Nicaragua 100,000 wameikimbia nchi yao. Wengi wao, takribani 75,000 walitafuta ukimbizi katika nchi iliytoko kusini mwa Nicaragua yaani Costa Rica. Kutokana na wanaowasili kuongezeka, UNHCR inategemea idadi ya raia wa Nicaragua wanaosaka hifadhi nchini Costa Rica kuongezeka kufikia 125,000 katika mwaka huu wa 2020.