Uhamiaji vijijini waweza kuleta tija ya maendeleo:IOM 

26 Machi 2020

Shirila la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema uhamiaji una mchango mkubwa katika kuleta maendeleo vijijini kupitia sekta ya kilimo hali ambayo inakuwa faina kwa wahamiaji na jamii zinazowahifadhi.

Huyo ni Gary muhamiaji kutoka Zimbabwe ambaye sasa anaishi Afrika Kusini akisema safari yake ilikuwa ngungu hasa ukizingatia Zimbabwe uchumi ulikuwa mbaya hakuna ajira, makampuni yanafungwa na hakukuwa na jinsi ya kujikimu akaamua kuhamia Zimbabwe kwenye sekta ya kilimo.

Kwa mujibu wa IOM barani Afrika kilimo ni sekta inayovutia wahamiaji wengi akiwemo Gary ambaye kwa sasa anafanya kazi kama meneja wa kitengo cha kufungasha bidhaa kwenye shamba kubwa la ndizi na nyanya mjini Komatpoort nchini Afrika Kusini

“Fursa yangu ya kwanza ilikuwa ni kuendesha tingatinga la kubeba mizigo kwa kuwa hiyo ndio kazi pekee iliyokuwepo, nilikuwa na uzoefu hapo kabla toka nyumbani, lakini pia nilikuwa na uzoefu kidogo wa kuchomelea masuala ya makenika nilikuwa naweza kufanya hizo kazi ndogondogo hivyo baada ya muda wakatambua kwamba huyu jamaa anaweza kuhimili ,sasa mie ni meneja nasimamia ufungashaji wa nyanya na ndizi.”

Gary anasema alipendelea kufanya kazi kwenye sekta ya kilimo kwa sababu ni kazi ambayo tayari alikuwa anaifahamu

“Kilimo nadhani ni sekta inayotoa ajira nyingi kuliko kazi nyingine yoyote na watu wanamudu kirahisi kilimo, wanajifunza haraka, kwa sababu kiko kila mahali hata majumbani kwao , vijijini kwao watu wanalima hata kama ni kilimo kidogo”

Hivi sasa Garry anasimamia wafanyakazi 200 katika kitengo chake na kipato anachopata kinamsaidia yeye na familia yake aliyoiacha Zimbabwe.

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO na IOM wanawachagiza wahamiaji kuingia katika sekta ya kilimo kwani jembe halimtupi mkulima

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter