Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda sasa ina wagonjwa 8 wa COVID-19, masoko yote yafungwa

Masoko yafungwa nchini Uganda wakati serikali ikichukua hatua kukabiliana na kusambaa kwa COVID-19.
UN News/ John Kibego
Masoko yafungwa nchini Uganda wakati serikali ikichukua hatua kukabiliana na kusambaa kwa COVID-19.

Uganda sasa ina wagonjwa 8 wa COVID-19, masoko yote yafungwa

Afya

Nchini Uganda serikali imeimarisha juhudi za kudhibiti virusi vya Corona COVID-19 baada ya kuthibitishwa kwa wagonjwa wapya wanane katika nchi hiyo na kuwaacha wananchi wakiwa katika hali ya taharuki. Miongoni mwa hatua mpya zilizochukuliwa sasa ni uamuzi wa kufunga masoko ambayo yalikuwa yameaachwa  wazi na kusababisha bei za bidhaa muhimu kupanda.

Wagonjwa hao wa COVID-19 waliothibitishwa mpaka sasa ni 9 akiwemo yule wa kwanza kabisa aliyetangazwa usiku wa kuamkia Jumapili 22 mwezi huu.

Baadhi ya wagonjwa nane hao wapya walisafiri kwenye ndege moja na yule wa kwanza lakini walikwenda majumbani kwani hawakubainika mapema.

Hofu imetanda na mamlaka wanachukua hatua zaidi ikiwemo kufungwa kwa dharura kwa masoko ya kila siku yaliokuwa yameaachwa. 

(Sauti ya mchuruzi akiondoka)

Katika mji wa Hoima soko la nguo la Hardware Marekt polisi limefungwa leo ambapo Tom Mpabaisi ni Mkuu wa kituo cha polisi cha Hoima.

CLIP:

Kando na hayo mamlaka za serikali ya Uamda zimesitishwa shughuli zote za uvuvi kwneye Ziwa Albert kutokana na utata wa kudhibiti wavuvi kwenye Ziwa hilo linalopakanisha Uganda an Jamhuri ya Kidemoktrasa ya Kongo (DRC). Maeneo ya mijini yameanza kukimbiwa na wananchi huku bei ya bidhaa ikipanda.

Serilkali inatoa wito kwa wanchi kuwa watulivu ikisema inafanya ikila iwezalo katika ushirikiano na wadau wake kudhibiti mlipuko huu.