Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamwe sitakata tamaa. Nitashinda!-Nakout Slylvia

Kijiji nchini Sudan Kusini, barabarani kati ya Yambio na Maridi, Equatoria ya Magharibi.
UN Photo/JC McIlwaine
Kijiji nchini Sudan Kusini, barabarani kati ya Yambio na Maridi, Equatoria ya Magharibi.

Kamwe sitakata tamaa. Nitashinda!-Nakout Slylvia

Wahamiaji na Wakimbizi

Nakout Sylvia alitekwa nyara na kikundi cha waasi cha Uganda mnamo 2003 na alikamatwa mateka kwa miaka 12 huko Afrika ya Kati. Kama matokeo ya unyanyasaji wa kijinsia wa kila mara, aliambukizwa Virusi Vya UKIMWI, VVU. Nakout baadaye alifanikiwa kutoroka na akapata hifadhi nchini Finland ambako sasa ameanza kujifunza mchezo wa gofu wa frisbee ambao ni maarufu nchini Finland. Je maisha yake hivi sasa yako vipi?

Nafikiri haya ni maisha bora ambayo nimewahi kuwa nayo tangu nimezaliwa.Niko imara, na wakati mwingine najihisi kama siumwi.

 

Ni Nakout mkimbizi kutoka Sudan Kusini anayeishi nchini Finland ameanza kujifunza kucheza fresbee golf, mchezo maarufu wa Gofu nchini Finland, anasema,“Inakufanya uwe  sawa kimwili na mwenye utulivu.Inaua msongo wa mawazo kwa namna unavyozunguka, zunguka. Unaporudi nyumbani, ukaoga maji baridi na kulala, unajisikia kuchoka sana.Ni mazoezi mazuri.”

Nakout alitekwa na waasi wa LRA mnamo mwaka 2003 na akateseka kwa miaka kwa manyanyaso ya kingono. Alitoroka na sasa anaishi na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI.

“Nilikuja Finland katika nyakati ambazo nilikuwa siwezi kulala. Nilikuwa nalala kwa kunywa dawa za usingizi. Hali yangu ya kiafya ilikuwa mbaya. Nilikuwa nazidiwa kila siku. Lakini tangu nilipowasili Finland tarehe 28 mwezi Mei mwaka jana, ninaona mabadiliko mengi.Ninaona bado nina matumaini ya maisha ndani yangu.”

Nakout ameanza kujifunza lugha ya kifin inayozungumzwa nchini Finland.Na anawafundisha lugha ya kiingereza wakimbizi wengine na katika video hii ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anaonekana akiwa katika shughuli yake hiyo ya kujifunza na kufundisha.

Na baadaye anaahidi kutoshindwa katika njia yake mpya ya kucheza Gofu.“Tulikuwa tunacheza watatu lakini mara zote wananishinda, kwa kuwa bado mimi ni mpya katika mchezo huu. Lakini sitakata tamaa. Ninawaahidi kuwa msimu wa kaingazi ujao, nitawashinda. Sina wasiwasi. Sikati tamaa. Ndiyo, siwezi.Sitakata tamaa hata iweje.”