Wanawake wafungwa nchini CAR wapatiwa mafunzo ya ujasiriamali:MINUSCA

10 Machi 2020

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ujulikanao kama MINUSCA kupitia programu zake za kuwawezesha wanawake unatoa mafunzo ya ujasiriliamali kwa wanawake wafungwa mjini Bangui ili waweze kukabiliana na hali ngumu gerezani.

Katika gereza la wanawake la Bimbo mjini Bangui afisa wa MINUSCA anayehusika na masuala ya haki na kubadili tabia, Aminata Diakhate, amewatembelea wafungwa wanawake kuzungumza nao ili kuwasaidia kukabiliana vyema na mazingira ya jela kwa sababu anasema, "pindi unapoingia jela tu watu huwa na kawaida ya kukubagua, sisi ambao tunafanya kazi jela tunapaswa kuwaonyesha wanawake hawa wafungwa kwamba jela sio mwisho wao. Kwa sababu uko jela haimanishi kwamba wewe ni mtu mbaya. Tunachagua wanawake kwa sababu ujumbe huu unawaingia kwa urahisi ambao ni waleta uhai na wakufunzi.”

Mbali ya elimu ya mdomo Aminata anasema wanapewa pia elimu ya vitendo kutengeneza vitu mbalimbali kama viatu, nguo, sabuni na pete za ufunguo, "mafunzo haya yanawafanya waweze kukabiliana na msongo wa mawazo wa jela, kwa sababu unapokuwa kifungoni na kuwekwa mahali pamoja siku nzima muda unakuwa mrefu sana. Wanaanza kuwa na mawazo mabaya, msongo wa mawazo na fatiki, hivyo ili kuepuka hayo wanawake wanajikita na shughuli hizo

Ameongeza kuwa mafunzo haya pia yana lengo la kusaidia kuwajumuisha tena katika jamii wanawake hawa pindi wanapotoka jela.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter