Visa vya COVID-19, Jumamosi hii vimefikia 100,000:WHO

7 Machi 2020

Idadi ya visa vya Corona, COVID19 vimepita laki moja kote duniani kwa mujibu wa taarifa ya shirika la afya duniani, WHO iliyotolewa Jumamosi.

Taarifa hiyo imesema “wakati tukabiliwa na wakati huu wa masikitiko na majonzi, WHO inazikumbusha nchi zote na jamii kwamba kusambaa kwa maambukizi haya kunaweza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa au hata kubadilishwa kabisa kwa kutekeleza shughuli na mikakati ya kuudhibiti ugonjwa huo”

Shirika hilo pia limezitaka nchi ziendelee na juhudi ambazo zimekuwa zikifanya kazi kudhibiti idadi ya visa na kupunguza maambukizi ya virusi hivyo ambayo vilibainika kwa mara ya kwanza Wuhan China mwezi Desemba mwaka jana.

Hatua hizo ni pamoja na kubaini watu ambao ni wagonjwa wa matatizo ya mfumo wa hewa na kuwapeleka kwenye huduma laki pia kufuatilia watu waliokutana nao, kuandaa vituo vya afya kuweza kuhimili wimbi la wagonjwa na kuwapa mafunzo wahudumu wa afya.

Taarifa imeongeza kuwa “kila juhudi inayofanyika ya kudhibiti virusi hivyo na kupunguza kasi ya maambukizi inaokoa maisha. Juhudi hizi zinaipa mifumo ya afya na jamii muda unahohitajika kujiandaa na watafiti muda zaidi wanaouhitaji kubaini dawa inayofanya kazi na kutengeneza chanjo.”

WHO itaendelea kufanyakazi kwa karibu nan chi na washirika wengine kuratibu hatua za kimataifa za kukabiliana na ugonjwa huuna kuandaa muongozo , kugawa vifaa vinavyohitajika na kujulisha umma jinsi ya kujilinda wao na kuwalinda wengine.

WHO imesisitiza kwamba “Ni lazima tusitishe, tuukabili, kuudhibiti, kuuchelewesha na kupunguza athari za virusi vya corona kila fursa tuipatayo. Kila mtu anaweza kuchangia iwe ni nyumbani, katika jamii, kwenye mfumo wa huduma ya afya, kazini au mwenye mfumo wa usafiri.”

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud