Usawa wa kijinsia ni faida kwa kila mtu:UN

8 Machi 2020

Faida za usawa wa kijinsia sio tu kwa wanawake na wasichana bali ni kwa kila mtu ambaye maisha yake yatabadilika kutokana na dunia yenye usawa.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women Phumzile Mlambo-Ngukca katika ujumbe wake wa siku ya wanawake duniani inayoadhiishwa leo.

Bi. Ngukca amesema kaulimbiu ya mwaka huu inahusu kizazi chenye usawa ambayo inajikita na masuala ya nayowakabili wanawake na wasichana vizazi na vizazi.

Ameongeza kuwa “hatuna usawa duniani hivi sasa na wanawake wanaghadhibishwa na kutiwa hofu na mustakbali wao, kimsingi hawana uvumilivu tena na mabadiliko n a ni kitu ambacho kimetawala maisha yao kwa muda mrefu.”

Bi. Mlambo-Ngukca amesisitiza kwamba wasichana wanahudhunishwa na hali ya dunia yetu, ukatili unaoelekezwa kwao na kasi ndogo ya mabadiliko katika masuala yanayowahusu kama elimu.

“Inayoniondoa uvulivu zaidi ni kasi ndogo ya kuleta usawa wa kiuchumi, ambayo ni kichocheo cha kurudia kwa umasikini.” Amesema mkuu huyo wa UN women.

Amesisitiza kwamba sera zinahitajika ambazo zinachagiza usawa katika huduma za msingi za kuhudumia watoto na kuhudumia familia lakini pia kwa wanaofanya kazi katika sekta zisizorasmi.

Hata hivyo Bi Ngukca amesema “pamoja na kupoteza uvumilivu kimsingi hatukati tamaa. Miaka 25 iliyopita imetudhihirishia nini kinachohitajika kuchapuza hatua kwa ajili ya usawa.””

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud