Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafunzo kutoka TAMWA-Zanzibar yawezesha wanawake wa Kidoti, Kaskazini A

Wanawake waliopokea mafunzo yaliyotolewa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania, TAMWA kuhusu kuweka na kukopa.
UN News/Assumpta Massoi
Wanawake waliopokea mafunzo yaliyotolewa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania, TAMWA kuhusu kuweka na kukopa.

Mafunzo kutoka TAMWA-Zanzibar yawezesha wanawake wa Kidoti, Kaskazini A

Wanawake

Huko Zanzibar, Tanzania mafunzo yaliyotolewa na chama cha wanahabari wanawake Tanzania, TAMWA kuhusu kuweka na kukopa yamewezesha wanachama wake ambao ni wanawake wakazi wa eneo la Kidoti, wilaya ya kaskazini A, kuweza kujiinua kiuchumi. 

Eneo la Kidoti, Wilaya ya Kaskazini A, kisiwani Unguja,  Zanzibar nchini Tanzania nakutana na wanakikundi cha Mwanzo Mgumu chenye wanachama 20.

Mafunzo kutoka chama cha wanahabari wanawake, Tanzania, TAMWA tawi la Zanzibar, kuhusu kuweka na kukopa yamewajengea uwezo wa kuweza hata kukopeshana na kufanya biashara.

Mchana huu nimekuta wanakikundi wakiwa katika siku ya kuweka hisa zao.

Nats..

Kuna kikoba cha fedha za kukopeshana na pia mfuko wa Jamii kwa ajili ya shughuli za kifamilia kama vile harusi au msiba.

Mwenyekiti wa kikundi hiki Fatuma Ally Heri akafunguka.

(Sauti ya Fatuma Ally Heri)

Fedha wanazokopeshana kutoka kwenye hisa huzitumia kuanzisha mradi kama anavyoelezea mwanachama huyu.

Hadi sasa mfuko wao walioanzisha miezi takribani 9 iliyopita sasa una zaidi ya shilingi Laki Nane.