Virusi vya Corona vyasababisha kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa CSW

4 Machi 2020

Virusi vya Corona au COVID-19 vimeendelea kuathiri shughuli a kiuchumi, kijamii na kisiasa duniani na athari hasi za hivi karibuni zaidi ni kuahirishwa kwa mkutano wa 64 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW uliokuwa ufanyike kwa wiki mbili hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuanzia tarehe 9 hadi 20 mwezi huu wa Machi.

Flora Nducha amefuatilia kwa kina mchakato wa kuahirishwa kwa mkutano huo na mbadala utakaofanyika kama anavyosimulia kwenye ripoti hii.

(Taarifa ya Flora Nducha)

(Sauti ya Stephane Dujarric)

"Mkutano huo wa siku moja utahusisha hotuba, kisha kufuatiwa na kupitishwa kwa rasimu ya azimio la kisiasa na rasiimu nyingine za maazimio. Kisha kikao hicho kitaahirishwa hadi itakapotangazwa tena. Hakutakuwepo na mjadala mkuu na wala matukio ya kando yanayoandaliwa na nchi wanachama na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Katibu Mkuu atahutubia kama ilivyopangwa tukio hilo."

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter