Mlo shuleni ni kichocheo cha maendeleo na ukuaji uchumi Afrika:WFP/FAO

3 Machi 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeungana na Muungano wa Afrika AU, na nchi kote barani Afrika kuadhimisha siku ya mlo shuleni likisisitiza kwamba uwekezaji katika nguvu kazi kupitia mipango ya afya na lishe bora mashuleni kunaweza kuleta faida kubwa zaidi ya kupata elimu. 

Kwa mujibu wa shirika hilo barani Afrika nyi nyingi zimefanya mlo shuleni kuwa ni paumbele cha taifa na watoto zaidi ya milioni 30 sasa wanafaidika programu ya mlo mashuleni barani humo. Kwa mfano Ghana, Malawi, Kenya na Zimbabwe zote zinalisha watoto Zaidi ya milioni moja huku Afrika Kusini na Nigeria lkila moja inalisha watoto Zaidi ya watoto milioni 9 kwa siku ya shule kwa mwaka mzima.

Kwan chi za Afrika Magharibi pekee serikali zinawekeza dola mil;ioni 500 kwa mwaka kwa ajili ya kuendesha mlo mashuleni. Akisisitiza kuhusu umuhimu wa uwekezaji huo mkurugenzi mtendaji wa WFP David Beasley amesema “ kuwekeza katika kizazi kijacho ni kuwekeza katika mustakabali wetu wa pamoja. Tunashuhudia jinsi gani programu za mlo mashuleni zinavyobadili maisha ya mamilioni ya wa watu barani Afrika na duniani kote, hususan kwa wasichana na kuwapa fursa za kufikia uwezo wao.”

Ameongeza kuwa mlo mashuleni unahakikisha kwamba watoto wana afya Njema na ustawi unaowawezesha kuhudhuria shule, kusoma, na kufikia uwezo wao wanapokuwa watu wazima.

Hata hivyo shirika hilo linasema kwa bahati mbayá leo hii kuna watoto milioni 73 wa shule kote duniani ambao wanakwenda shule na njaa ambapo kati yao milioni 61 wako barani Afrika.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter