Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuhukumiwa kwa wanamgambo CAR ni ishara ya kutendeka kwa haki:Lt jenerali Keita

Luteni Jenerali Balla Keita kutoka nchini Senegal ambaye ni kamanda anyeondoka wa vikosi vya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA..
UN News/Dianne Penn
Luteni Jenerali Balla Keita kutoka nchini Senegal ambaye ni kamanda anyeondoka wa vikosi vya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA..

Kuhukumiwa kwa wanamgambo CAR ni ishara ya kutendeka kwa haki:Lt jenerali Keita

Haki za binadamu

Hatua ya hivi karibuni ya kuwahukumu wajumbe wa kundi la wanamgambo nchini Jamhuri ya afrika ya Kati CAR, kutokana na mauaji ya raia na walinmda amani yalitotekelezwa mwaka 2017 imetoa ujumbe mzito kwamba ukwepaji sheria hauvumiliki. 

Kauli hiyo imetolewa na Luteni Jenerali Balla Keita kutoka nchini Senegal ambaye ni kamanda anyeondoka wa vikosi vya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA.

Kamanda ameyasema hayo alipozungumza mjini New York na UN News kuhusu hukumu hiyo dhidi ya wanamgambo, na masuala mengine kama athari za mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka jana baina ya serikali na makundi 14 yenye silaha na kuongezeka kwa uungaji mkono wa kimataifa kuhusu mkakati wa Umoja wa Mataifa wa hatua kwa ajili ya operesheni za ulinzi wa amani.

Luten Jenerali Keita mwenye uzoefu wa miaka 45 katika jeshi na operesheni za ulinzi wa amani kwanza anaeleza kwa MINUSCA umuhimu wa mkataba huo wa amani,“Kwa hakina nina furaha kwamba tumefikia muafaka wa amani , kama unavyojua hakuna suluhu nyingine kama suluhu ya kisiasa. Kwetu ni kitu kizuri lakini kinaongeza kazi nyingine kwa vikosi vyetu kwa sababu mbali ya wajibu wetu wa kulinda raia na taasisi zao pia tunahitaji kuulinda mkataba wa amani na kuhakikisha unafanyakazi na tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha makundi yenye silaha yanasalia ndani ya mkataba huo wa amani.”

Na kuhusu hukumu dhidi ya wanamgambo waliotekeleza mauaji huko Bangassou amesema, “Tumepoteza takriban walinda amani 12 katika tukio hilo la Bangassou hao ni wengi sana, angalau sehemu ya wanamgambo hao wamehukumiwa , hivyo haki imetendeka na nadhani ni ujumbe mzuri kwa watu wote wabaya kuwajuza kwamba chochote unachofanya utalipa gharama siku moja, hautokwepa sheria kwa muda mrefu .”

Ameongeza kuwa mpango wa MINUSCA utaendelea kufanya kila uwezalo kuhakikisha amani inarejea CAR na raia wanalindwa.