Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya walio hatarini kukumbwa na njaa yaongezeka Sudan Kusini

Familia nyingi zilizokimbia makazi yao huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria kwa hofu ya magaidi wa Boko Haram zinakabiliwa na njaa.
OCHA/Franck Kuwonu
Familia nyingi zilizokimbia makazi yao huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria kwa hofu ya magaidi wa Boko Haram zinakabiliwa na njaa.

Idadi ya walio hatarini kukumbwa na njaa yaongezeka Sudan Kusini

Msaada wa Kibinadamu

Takribani watu milioni 6.5 nchini Sudan Kusini, ambao ni zaidi ya nusu ya watu wote wa Sudan Kusini, wanaweza kuwa hatarini kukumbwa na baa la njaa katika miezi ya Mei na Julai, yameonya mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya pamoja iliyotolewa leo ya mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Chakula na kilimo FAO, la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Sudan Kusini, hali inaleta wasiwasi mkubwa katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko makubwa mwaka jana wa 2019 ambako uhakika wa chakula umedorora tangu mwezi Juni.

Watu ambao wako katika hatari zaidi wanafikia 20,000 ambao hadi kufika mwezi wa April watakuwa wanateseka kutokana na kiwango cha juu kabisa cha njaa ambacho kitaalamu kinawekwa katika ngazi ya IPC 5 ni wale ambao wanaishoi katika maeneo ya Akobo, Duk na Ayod, maeneo ambayo yaliathiriwa sana na mvua kubwa mwaka jana na wanahitaji msaada wa kibinadamu wa  haraka na endelevu.

Inakadiriwa kuwa njaa itaongezeka zaidi kati ya sasa na mwezi Julai hususani katika maeneo ya Jonglei, Upper Nile, Warrap na Kasikazini mwa Bar el-Ghazal ambako kuna zaidi ya watu milioni 1.7 wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula uliofikia ngazi ya tatu yaani IPC 4 kutokana na mafuriko na viwango vidogo vya uzalishaji wa chakula. Kauti 34 zitafikia ngazi ya dharura ya ukosefu wa chakula wakati wa msimu wa njaa tangu mwezi tarehe 15 ya mwezi Januari.

Taarifa imesema, kiujumla, mwezi wa Januari mwaka huu, watu milioni 5.3 wa Sudan Kusini walikuwa tayari wanahangaika kuweza kujipatia chakula chao wenyewe au walikuwa katika janga la ukosefu wa chakula la ngazi ya 3 yaani IPC 3 na zaidi.

Ripoti hiyo inaeleza pia kuwa hali ni mbayá kwa watoto kwani takribani watoto milioni 1.3 wataathirika na utapiamlo mkali katika mwaka huu wa 2020.