Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Al Hassan anayo kesi ya kujibu-ICC

Al Hassan akiwa mbele ya mahakama ya ya kimataifa ya uhalifu, ICC mnamo Aprili 4, 2018
ICC-CPI
Al Hassan akiwa mbele ya mahakama ya ya kimataifa ya uhalifu, ICC mnamo Aprili 4, 2018

Al Hassan anayo kesi ya kujibu-ICC

Haki za binadamu

Baraza la rufaa la Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC limeitupilia mbali rufaa iliyokuwa imeletwa mbele yao na  Al Hassan kupinga uamuzi wa awali wa kumpata na kesi ya kujibu kuhusu makosa anayodaiwa kuyatenda katika eneo la Timbuktu nchini Mali kati ya mwaka 2012 na 2013.

ICC imesema Al Hassan ambaye pia anafahamika kama Abdoul Aziz, Mohamed, Mahmoud, makosa yaliyotambuliwa katika uamuzi wa awali wa tarehe 27 mwezi Septemba 2019 yalikuwa mazito kiasi cha kuhalilisha maamuzi ya mahakama.

Mahakama ilikuwa imekubaliana tangu wakati huo kuwa anayo kesi ya kujibu kutokana na makosa anayohusishwa nayo.

Kwa mujibu wa ICC, kuanzia mwezi Aprili 2012 hadi Januari 2013, wakati Timbuktu ilikuwa chini ya miliki ya Al Qaeda katika makundi ya Islamic Maghreb (AQIM) na Ansar Eddine, Bwana Al Hassan, “anaweza kuwa alishiriki jukumu la kuongoza kutekeleza uhalifu na mateso yaliyolenga dini na jinsia yaliyotekelezwa na makundi ya watu wenye kujihami kwa silaha dhidi ya raia.” 

Al Hassan, inadaiwa, pamoja na makosa mengine, alishiriki katika uharibifu wa makaburi ya watakatifu wa kiislamu huko Timbuktu na akashiriki katika sera ya kulazimisha ndoa ambayo wanawake wa Timbuktu walikuwa waathirika na iliyosababisha vitendo vya ubakwaji vya mara kwa mara n ahata kufikia kuwafanya kuwa watumwa wa kingono.

Usikilizwaji wa kesi umepangwa kuanza tarehe 14 ya mwezi Julai mwaka huu wa 2020.

 

TAGS: Sheria na kuzuia uhalifu, ICC, Al Hassan, Timbuktu, Islamic Maghreb, AL Qaeda, AQIM, Ansar Eddine