Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa ProPESCA wabadili maisha ya wavuvi Msumbiji:IFAD

Wavuvi kutoka Kenya wakiwa katika harakati za uvuvi kwenye ziwa Victoria ambako Sangara ndiko makazi yake zaidi
FAO/Ami Vitale
Wavuvi kutoka Kenya wakiwa katika harakati za uvuvi kwenye ziwa Victoria ambako Sangara ndiko makazi yake zaidi

Mradi wa ProPESCA wabadili maisha ya wavuvi Msumbiji:IFAD

Tabianchi na mazingira

Mradi unaoendesha na mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD ujulikanao kama ProPESCA umebadili maisha ya wavuvi wengi wanaoshi katika mwambao wa Msumbiji waliohofia uvuvi wa kupindukia na mabadiliko ya tabianchi.

Karibu katika Kijiji cha Zalala kwenye pwani ya mchanga ya Msumbiji ni Kijiji kidogo lakini kilichosheheni mambo mengi , wakazi wake kwa asilimia kubwa ni wavuvi , na uvuvi ambao ni sehemu huchangia asilimia kubwa ya uchumi wa taifa hili.

Lakini kwa mujibu wa IFAD siku za hivi karibuni hali imeanza kubadilika kutokana na uvuvi wa kupindukia, mahitaji mengi kupita uwezo na mabadiliko ya tabianchi na kuwa tishio kubwa kwa uchumi , maendeleo na Maisha ya wakazi wa eneo hili.

Na ndio mradi wa ProPESCA ulianzishwa na IFAD ilikusaidiana na serikali ya Msumbiji kushughulikia changamoto hizo katika majimbo yote saba yaliyo kwenye mwambao wa nchi hiyo wakizishirikisha jamii kwa kuwapa mafunzo uvuvi wa msimu, ukaushaji wa samaki na njia nyingine za kuhifadhi samaki kwa muda mrefu.

zaidi ya watu 280,000 wamepata mafunzo na zaidi ya nusu ya watu hao ni wanawake, miongoni mwao ni Mariamo Fermino

(SAUTI YA MARIAMO FERMINO)

“Naitwa Mariamo niña umri wa miaka 27, ni mwanamke mfanyabiashara ya ujasiriliamali, nachuuza samaki wabichi na waliokaushwa kwa chumvi”

Mariamo alihamia Zalala mwaka 2013, akianza na biashara ya kuuza soda na keki kwa wavuvi, lakini sasa asante kwa mafunzo ya ProPESCA na warsha zake biashara yake ikakuwa na kugeuka ya samaki

(SAUTI YA MARIAMO FERMINO)

Mradi wa ProPESCA umetusaidia na kubadili maisha yetu ili tuweze kusaidia familia zetu. Katika mradi huu nimejifunza kukausha samaki kwa kutumia chumvi, nimejifunza ni nyavu gani za kutumia na nyavu aina gani zinaruhusiwa wakati wa msimu wa uvuvi.”

Mariamo amejifunza pia kupika na hata kuoka keki za samaki na sasa kajiunga kwenye chama.

(SAUTI YA MARIAMO FERMINO)

“Mradi umenisaidia kujiunga kwenye ushirika . Tuko wanawake 10 tunaochuuza samaki, nimejifunza kutengeneza pesa.”

IFAD inasema mbali ya kubadili maisha mradi huo umesaidia maendeleo ya kiuchumi kutokana na uuzaji wa samaki, kuboresha miundombinu ya biashara, kuimarisha taasisi na kuboresha lishe.