Ni wakati wa dunia kufuata nyayo za Pakistan kuhusu wakimbizi:Guterres 

Katibu Mkuu António Guterres (kushoto) na Shah Mehmood Qureshion, waziri mkuu wa Pakistan (Kulia) wakizungumza na waandishi wa habari mjini Islamabad
May Yaacoub/UN News
Katibu Mkuu António Guterres (kushoto) na Shah Mehmood Qureshion, waziri mkuu wa Pakistan (Kulia) wakizungumza na waandishi wa habari mjini Islamabad

Ni wakati wa dunia kufuata nyayo za Pakistan kuhusu wakimbizi:Guterres 

Wahamiaji na Wakimbizi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres amesema anaamini kwa dhati kuwa huu ni wakati wa dunia kutafakari na kuiangalia Pakistan katika wigo mpana zaidi na kufuata nyayo zake hasa katika suala la kukirimu wakimbizi. 

Katika mkutano wa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Shah Mehmood Quaresh mbele ya waandishi wa habari mjini Islamabad Pakistan hii leo Guterres amesema “Ni kutambua ukarimu mkubwa na mshikamano wa Pakistan kwa miaongo kadhaa sasa na kuitanabaisha nafasi yake katika kukabili moja ya changamoto kubwa kabisa ya kimataifa inayoighubika dunia hivi sasa. Moja ya lengo kubwa la safari yangu ni kuidhihirisha Pakistan pamoja na yote yanayowezekana na uwezo wake.” 

Katibu Mkuu amesema hayo yote mizizi yake ni utamaduni wa taifa hilo kuanzia maono ya Muhammad Ali Jinnah hadi philosifia ya Allama Iqbal mpaka muziki wa Nusrat Fateh Ali Khan. 
Pia amesema ujasiri wa watu hao mfano Malala Yousafzai hadi utu wa Abdul Sattaar Edhi lakini pia sanaa na uchagizaji wa Sharmeen Obaid Chinoy. 

Pia amesema kwa siku za nyuma hata kwenye muichezo kama timu ya Pakistan ya Kriketi ya wanaume na wanawake. La muhimu Guterres amesema “Hapa Pakistan tunaona mshikamano, leo hii Pakistan ni nchi ya pili duniani kwa kuhifadhi wakimbizi wengi na kwa miongo kadhaa ilikuwa ni ya kwanza.” 


Miongo 4 ya kuhifadhi wakimbizi 

Kesho Jumatatu itakuwa ni miongo minne ya taifa hilo kuhifadhi wakimbizi kutoka Afghanistan. 
“Kwa miaka 40 licha ya changamoto zake Pakistan imekuwa ikihifadhi na kuwalinda wakimbizi toka Afghanistan, huku ikipatiwa msaada kidogo sanakutoka jumuiya ya kimataifa. Ninaweza kuwa shahidi katika hili , nikihudumu kama kamishina mkuu wa wakimbizi wakati wote niliiona 
Pakistan kama mshirika wa kuaminika na mkarimu” 

Amesema mtu anaweza kufikiria bila msaada na ukaribu wa Pakistan wakimbizi wa afghanistan wangrekuaje leo hii. 
Ameaidi kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia Pakistan na “natoa wito kwa nchi zingine kuisaidia Pakistan na pia kuonyesha uongozi kama wake wa kushirikiana jukumu hili kwenye ukanda huu na duniani kote.” 

Katibu Mkuu Antonio Guterres (katikati) akishiriki katika sherehe ya upandaji miti akiwa na Makhdoom Shah Hussain Qureshi waziri wa mambo ya nje wa Pakistan
Mark Garten).
Katibu Mkuu Antonio Guterres (katikati) akishiriki katika sherehe ya upandaji miti akiwa na Makhdoom Shah Hussain Qureshi waziri wa mambo ya nje wa Pakistan

Amani na usalama 

Kuhusu suala la amani na usalama Katibu Mkuu amesema Umoja wa Mataifa unashukuru ahadi na dhamira ya Pakistan katika kuchangia walinda amani. 
Amesema kwa muda sasa Pakistan imekuwa mmiongoni mwa wachangiaji wakubwa duniani wa operesheni za ulinzi wa amani za umoja wa Mataifa ikiwa na zaidi ya wanaumme na wanawake 4000 katika operesheni 9 za Umoja wa Mataifa kote duniani. 
Katibu Mkuu ameshukuru uungaji mkono wa serikali hiyo mkakati wa Umoja wa Mataifa wa hatua kwa ajili ya ulinzi wa amani na pia kwa ahadi yake ya kuendelea kuboresha ufanisi wa operesheni za aulinzi wa amani za umoja wa Mataifa. 

 Mvutano Kashmir 

Katibu mkuu amesema yeye na waziri mkuu Quaresh wamejadili suala la usalama kanda ya Asia kusini. Na kuhusu suala la Jammu na Kashmir Guterres ameishukuru kazi inayofanywa na jeshi la uangalizi la Umoja wa Mataifa nchini India na Pakistan. 
Amesema jeshi hilo UNMOGIP litaendelea kufuatilia usitishaji uhasama kwenye msitari wa udhibiti kwa mujibu wa jukumu lake na leo Katibu Mkuu amezindua makao makuu mapya ya mpango huo. 
Hata hivyo Guterres amesema “Nina wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa mvutano ambao tuliushuhudia mwaka jana. Mara kadhaa nimerejea kusisitiza umuhimu wa kujizuia na kuchukua hatua za kusitisha uhasama zote za kijeshi na mazungumzo, huku nikiendelea kujitolea kusaidia pande zote endapo zitataka msaada wa ofisi yangu.” 
Amesisitiza kwamba diplomasia na majadiliano vinasalia kuwa nyenzo pekee ya kuahakikisha amani na utulivu na suluhu kwa kuzingatia katika ya Umoja wa mataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 
Amerejelea kuhimiza kwamba katika hali yoyote ile ya mvutano na machafuko ni muhimu kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa na kuzingatia misingi yote ya uhuru. 

Kuhusu Afghanistan 

Akigeukia Afghanistan, guterres amesema anafuatilia kwa karibu juhudi za kuleta amani nchini humo. Akisema kufikia suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Afghanistan ni muhimu sana kwa ajili ya kuokoa maisha na kusongesha mbele maendeleo endelevu. 
“Ni matumaini yangu kwamba majadiliano yatazaa matunda katika kuelekea kupunguza machafuko hususani yanayoathiri raia. Kupunguza machafuko ni muhimu katika kujenga kujiamini na msaada kwa ajili ya mchakato wa amani ambao utapelekea suluhu ya kudumu ya kisiasa na ukomeshaji kabisa mapigano.” 
Amesema mazingira hayo yatachangia kuwezesha kurejea kwa amani majumbani kwao maelfu ya watu na wakimbizi waliotawanywa. Amesema “Nataka kusisitiza kwamba suluhu tutaoipendelea ya kudumu kwa suala la wakimbizi kila wakati imekuwa kurejea kwa hiyari na kwa usalana na utu kwenye nchi walikotoka, na hili pia ni kwa wakimbizi wa Afghanistan” .
Katibu Mkuu amesema kupitia msaada wa juhudi za amani zinazoendelea na ujenzi wa mazingira ya muafaka wa kikanda , Pakistan inaendelea kuwa na jukumu muhimu katika ufikiaji wa fursa hii ya kihistoria kwa jili ya amani. 
Amesisitiza kwamba Umoja wa Mataifa unasiamamia ahadi yake ya kuunga mkono mchakato wa amani jumuishi na unaoongozwa na Waafghanistan wenyewe ambao unaheshimu haki za binadamu na kuelekea katika amani endelebu Afghanistan. 
Katika Mkutano huo na waandishi wa habari Katibu mkuu amegusia tena suala la changamoto ya mabadiliko ya tabianchi akisema Pakistan iko miongoni wa waathirika wa mstari wa mbele wa mabadiliko ya tabianchi. Amekaribisha mradi wa kampeni ya tsunami wa upandaji miti bilioni 10 na miradi mingine. 
Na kukabiliana mabadiliko ya tabia nchi Guterres ameahidi kuendelea kushinikiza hatua za kudhibiti ongezeko la joto duniani lisizidi nyuzi joto 1.5, na hii ikimaanisha kwamba kufikia dunia huru bila hewa ukaa ifikapo 2050. 
Na mwisho amesema anataka kutambua ahadi ya Pakistan ya utekelezaji wa ajenda ya 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu SDGs, mkakati wa kimataifa wa kutokomeza uamsikini , kufikia usawa wa kijinsia, kulinda mazingira na kujenga utandawazi wenye usawa unaofanya kazi kwa wote. 
Amesema Pakistan ilikuwa msitari wa mbele katika kujumuisha SDGs katika ajenda yake ya kimataifa ya maendeleo. 

Maswali na majibu

Kisha Katibu Mkuu na waziri mkuu Quaresh wakapata fursa ya kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari. Alipoulizwa kuhusu hatua gani yeye na umoja wa Mataifa watachukua kuhusu suluhu ya suala la Kashmir Katibu Mkuu akajibu”Kwanza kabisa tangu mwanzo nimejitolea pamoja na ofisi yangu kuhusu kusaka suluhu ya suala hili na bila shaka ofisi yangu inaweza kufanya vizuri endapo itakubalika na pande zote. Kwa upande mmoja naamini kwamba kuna mchango mkubwa katika kufafanua nini kilichotokea kutokana na ripoti iliyotajwa na Kamishina mkuu wa haki za binadamu. Na kwa upande mwingine ni bayana kwamba tumechukua msimamo kuhusu haja ya maazimio ya Baraza la Usalama kutekelezwa na usitishaji uhasama mazungumzo yanayohuasiana na suala hilo, na suala lingine muhimun sana ambalo ni kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa msingi Jammu na Kashmir. 
Katibu Mkuu yuko Pakistan kwa ziara ya siku tatu ambayo itakunja jamvi tarehe 19 Februari.